REGINA MAGOKE (MUHAS): Afunguka Umuhimu wa mazingira safi eneo la biashara

REGINA MAGOKE (MUHAS): Afunguka Umuhimu wa mazingira safi eneo la biashara

Mazingira ni kitu chochote kinachomzunguka kiumbe hai na kisicho hai pamoja na maumbile yake.

Neno mazingira ubeba uhalisia wa sehemu husika katika eneo au sehemu ambapo shughuli kadhawakadha ingaliweza kufanyika.

Umuhimu wa mazingira safi katika shughuli mbalimbali mfano biashara kama vile upishi huitaji mazingira yaliyo safi na salama kwaajilii ya usalama wa afya za wanajamiii wa eneo husika, pamoja na watumiaji wa chakula hicho.

Katika mazingira yetu ndipo shughuli mbalimbali hufanyika ikiwa nikatika kuleta chachu ya maendeleo.

Leo tupo na Regina Magoke mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kwa fani ya afya ya mazingira (MUHAS) pia ni mpambanaji aliye na shauku katika nyanja mbali mbali kama vile uongozi,  afya, mazingira na jinsia kujishughulisha na mambo mbalimbali kwaajili ya maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Magoke atatuelezea kuhusu umuhimu wa mazingira bora/safi katika eneo lako la biashara. Kwa siku hizi za karibuni watu wamekuwa wakijisahau sana katika kuboresha mazingira yao wanayo fanyia biashara .

 

Anasema biashara mbalimbali zinazofanywa na watu wengi katika jamii zetu na taifa kwa ujumla huitaji ubunifu wa hali ya juu ili kuleta athari pamoja na mabaidiliko chanya kwenye biashara hizo.

Anafunguka na kueleza mojawapo wa ubunifu huo ni uendeshaji wa biashara katika mazingira safi na salama kwasababu zifuatazo,

Husaidia kuepuka milipuko wa magonjwa

Anasema uwepo wa mazingira safi na salama katika eneo la biashara husaidia kuepukana na mlipuko wa magonjwa mfano Chorela, ugonjwa ambao husambazwa na nzi kutokana na hali ya uchafu.

“Husaidia kuepukana na faini, mfano tozo zisizo tarajiwa, hiii inatokana na hali ya ukaguzi unaofanywa na wadau wa afya (Maafsa afya) pindi wanakagau na kukuta eneo lako la biashara si safi na salama hupelekea hali ya kutokutozwa faini,” anasema  

Magoke anasema mazingira safi uwavutia wateja na kuwafanya wanufaike na kutosheka na bidhaa zitolewazo kutoka kwa muhusika na hiyo ni kwasababu mazingira yapo safi na salama hali inayolinda afya ya mwanadamu katika nyanja mbalimbali.

 

“Husababisha uwepo na kuzaliwa kwa biashara nyingine nyingi zaidi, hii ni kwa sababu mazingira yamepewa kipaumbele katika utunzaji na husababisha kufanyika kwa shughuli nyingine nyingii zaidi,” anasema

Ushauri wake kwa Serikali katika kuboresha mazingira nchini

Ndani ya Mwananchi scoop, Magoke alifunguka na kutoa ushauri ka Serikali ambapo ameiomba ifanye uchunguzi wa kina katika maeneo mbalimbali ya wafanyabiashara ili kujua kiini cha watu kutopenda kufanya usafi.

“Naiomba Serikali yangu chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia viongozi wake wa serikali za mitaa na hata tawala za mikoa kuhakikisha wanafanya uchunguzi wa kina katika maeneo mbalimbali ya wafanya biasharaili kubaini sababu zinazofanya kampeni ya usafi kutofanikiwa.

“Pia iendelee kutoa elimu kwa jamii hasa wafanyabiashara juu ya umuhimu wa usafi wa mazingira katika biashara zao na athari chanya zitokeazo kwa kutofanya usafi wa mazingira hayo” amesema Magoke

Alimalizia kwa kusema “Pamoja na ziara za viongozi katika ukaguzi wa mazingira kwenye maeneo ya biashara faini zitozwe kwa yoyote atakaye kiuka sheria na taratibu za utunzaji wa mazingira katika maeneo ya biashara.

Pia ninaiomba serikali kupitia Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ikiongozwa na waziri Suleiman Jaffo kutekeleza hayo kwa weledi” anasema Magoke

Mwanadada Magoke amefunguka pia mbali na kusoma masuala ya sayansi pia anatamani kuwa kama Rais Samia kwa sababu ni kiongozi wa mfano wa kuigwa na wasichana wengi hapa nchini.

Anasema Rais Samia ameionesha dunia kuwa wanawake wakipatia nafasi za uongozi ngazi za juu wanaweza kufanya mambo makubwa na yenye manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla.

“.Ninatamani sana kuwa kama Rais Samia Suluh Hassan kwasababu ni kiongozi wa kuigwa anajikita katika harakati za maendeleo ya watanzania na ulimwenguni kote, Uongozi ni dhamana nami matamanio yangu kufika alipofika yeye,” anasema Magoke

Hata hivyo alisisitiza kuwa “Mazingira ni yetu sote hususani Katika biashara mbalimbali zinazofanyika ikiwa ni chachu ya maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla, usafi wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi katika taifa letu, hivyo tutunze mazingira kwaajili ya kulinda afya zetu.

“Na siku zote ukiweka mazingira ya biashara yako safi na salama ndo mwanzo wakuongeza wateja maana wateja wengi hupendelea mazingira yaliyo safi na salama kwao,” anasema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags