Rais Hakainde: Acheni kupeleleza simu za wapenzi wenu

Rais Hakainde: Acheni kupeleleza simu za wapenzi wenu

Rais nchini Zambia, Hakainde Hichilema amewataka raia wa nchi hiyo kuacha kuchunguza simu za wenzi wao na maoni hayo yamekuja kwa kujaribu kupunguza viwango vya talaka nchini.

Rekodi zinaonyesha nchini humo ilirekodiwa zaidi ya kesi 22,000 za talaka mwaka jana pekee, takwimu ambazo Rais alizitaja kuwa za kusikitisha.

Ukosefu wa haki za ndoa, uzinzi, unyanyasaji wa kijinsia, matusi na ukatili ni miongoni mwa sababu kuu za watu waliotajwa katika mahakama za kutaka talaka.

"Tunaoana kwa ajili ya mapenzi, hatuoi ili kwenda kuangaliana, au kwenda kunyoosheana kidole," Bw Hichilema alinukuliwa na vyombo vya habari akisema alipomkaribisha mfalme wa eneo hilo.

Inaripotiwa kwamba aliongeza: "Uhuru unamaanisha uwajibikaji katika kuweka mipaka uhuru wetu, si kuchezea uhuru wa wengine. Kuwa mvumilivu, uwe mwenye kuelewa."

Takwimu za miezi 12 iliyopita zilionyesha ndoa fupi zaidi nchini humo ilidumu kwa siku 30 huku ndefu zaidi ikiwa ni miaka 65.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post