Raia wa Morocco waandamana

Raia wa Morocco waandamana

Mamia ya watu waliandamana nchini Morocco siku ya Jumapili katika mji mkuu wa kiuchumi Casablanca kupinga kupanda kwa gharama za maisha katika taifa hilo na kutaka hatua zichukuliwe na serikali.

Waandamanaji hao kutoka chama cha Democratic Labour Confederation (CDT) walikusanyika katika uwanja wa kihistoria wa Casablanca wakielezea kutoridhishwa na kupanda kwa bei pamoja na kupunguzwa uwezo wa ununuzi.

Moja ya chombo cha habari nchini humo walishuhudia makabiliano kati ya maafisa wa usalama na waandamanaji lakini walisema maandamano hayo yalimalizika bila ya kutokea tukio kubwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags