Omondi aitaka serikali ya Kenya kuwajali wananchi wake

Omondi aitaka serikali ya Kenya kuwajali wananchi wake

Mchekeshaji kutoka Kenya Eric Omondi amewalipia billi akina mama wa tano waliokuwa kidaiwa katika hospitali waliojifungulia, baada ya kujua kuwa baadhi yao walikuwa na madeni katika Hospitali ya Pumwani nchini humo huku awasaidia wa mama hao bili walio kuwa wakidaiwa.

Omondi alitoa wito kwa Rais William Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua kuingilia kati na kuamru kuachiliwa kwa wanawake wengine waliozuiliwa kote nchini.

Inasemekana kuwa wanawake hao walikuwa wamezuiliwa katika kituo hicho cha matibabu kwa kushindwa kulipa bili zao za hospitali, huku baadhi yao wakishikiliwa kwa wiki kadhaa licha ya kuwa sawa kiafya.

Omondi ambaye amekuwa akipigania masuala ya kijamii yanayoathiri wakenya alijitokeza kwenye mitandao wa kijamii wa Instagram kwa  kuhamasisha umma kuhusu masaibu ya kina mama waliozuiliwa katika hospitali hiyo.

Kufuatia mtandao wake wa Instagram alifunguka na kusema kuwa “ Nimewachilia akina mama wachanga 5 waliokuwa wamezuiliwa Pumwani, Mheshimiwa Rais kabla hujalipa mabilioni ya shilingi 50 za CAS na kabla ya serikali kununua magari mapya kabisa kwa watendaji, tafadhali toa agizo kwa kina mama wote wanaozuiliwa hospital na kote nchini kuaachiliwa” Amesema Omondi

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags