Nyama ya nguruwe kujumuishwa kwenye chakula shuleni

Nyama ya nguruwe kujumuishwa kwenye chakula shuleni

Mipango inaendelea ya kuwezesha shule kujumuisha nyama ya nguruwe katika ratiba ya chakula nchini Rwanda kama njia ya kutokomeza utapiamlo.

Olivier Kamana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Rasilimali Wanyama amenukuliwa na gazeti la New Time nchini humo akisema.

“Tunaziomba shule kuanzisha miradi ya ufugaji wa nguruwe ili kuweza kumudu nyama ya nguruwe," alisema.

Mnamo mwaka wa 2019, mpango wa lishe shuleni ulitekelezwa katika shule za sekondari (zinazosaidiwa na serikali na za serikali) huku wanafunzi 680,000 wakipokea ruzuku ya Serikali ya chakula cha shule.

Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa shule za msingi na sekondari ziliongezeka kutoka 2,877 mwaka 2017 hadi 2,963.

Mnamo 2021, Rwanda ilizalisha tani 185,989 za nyama. Idadi ya nguruwe imeongezeka kutoka 989,000 mnamo 2012 hadi takriban milioni 1.5 mnamo 2021.

Nchi hiyo iilizalisha wastani wa tani 23,000 za nyama ya nguruwe kwa katika mwaka 2019 na inalenga kuongeza uzalishaji wa nyama hiyo hadi kufikia tani 68,000 ifikapo 2024.

“Tunashughulikia mpango wa kutumia vyanzo mbadala vya protini kulisha mifugo badala ya mahindi. Hii itasaidia kuongeza idadi ya wafugaji wa nguruwe na uzalishaji wa nguruwe,” alisema Kamana

 Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags