Nchi 6 Afrika zatuma maombi ya kuandaa AFCON 2027

Nchi 6 Afrika zatuma maombi ya kuandaa AFCON 2027

Nchi 6 zimetuma maombi ya kuwa mwenyeji wa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 ambazo ni Algeria, Botswana na Misri huku Kenya, Uganda na Tanzania zikiwasilisha maombi ya kuandaa kwa pamoja.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) tayari limepokea maombi na hatua inayofuata ni kuwasilisha zabuni ya mwisho Mei 23, 2023 ikijumuisha nyaraka zote (makubaliano ya uenyeji, makubaliano ya miji mwenyeji na dhamana ya Serikali)

Aidha ukaguzi utafanyika Juni 1-15, 2023 na uamuzi wa nani atakuwa mwenyeji utafanywa na kamati ya Utendaji ya CAF






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags