Nandy afunguka kuwa mkubwa kwa Billnass

Nandy Afunguka Kuwa Mkubwa Kwa Billnass

Ebwana eeh moja kati ya taarifa ambayo imekua gumzo kwenye mitandao ya kijamiini hii hapa inayowahusu wawili hawa Nandy pamoja na mume wake Billnass ambapo inasemekana kuwa bibie Nandy amemzidi umri mume wake.

Baada ya minong’ono na maneno ya chini chini African Princess ameamua kufunguka na kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo wakati akifanyiwa mahojiano na chombo cha habari hapa nchini.

 Nandy ameweka wazi kuwa licha ya kumzidi kiumri mumewe Billnass, uwezo wake wa kufikiri ni mkubwa mno kiasi cha kumfanya yeye kama nguzo na muongozo katika maisha yao!

“Almost tuko sawa mimi nimezaliwa  mwaka 1992 yeye 1993 tumepishana miezi 5 tu, simsifii lakini mume wangu ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana wa kufikiri anaweza kukaa na watu wa kubwa na akatoa mawazo yaani ana uwezo mkubwa ukilinganisha na umri wake.”

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post