Namna ya kutengeneza sabuni ya magadi kwa ajili biashara

Namna ya kutengeneza sabuni ya magadi kwa ajili biashara

Hellow! Natumai ni wazima wa afya wanangu wa nguvu, sasa leo tumekuja na suluhisho ambalo litakufanya kupata kipato ukiwa nymbani tu, hapa nazungumza na wale wamama ambao hawana kazi wako tu nyumbani, wanaweza kujishughulisha kwa kufanya biashara ya kuuza sabuni za magadi.

 

Yes, leo nimekusogezea mafunzo ambayo yataweza kukusaidia wewe kwa kutimiza mahitaji yako kwa kufanya biashara ndogo tu ambayo utaamua kuanzisha, sio ngumu sana kutengeneza sabuni hizi ukiamua kufanya basi unaweza ungana nami katika maelekezo haya, naamni utapata mwanga. 

 

Mahitaji
Caustic Soda kilo 3
Mafuta ya mawese lita 20
Sodium Silket
Maji lita 10
Rangi ya bluu vijiko 3

Jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua

1) Chukua coustic soda, changanya na maji na uanze kukoroga kuelekea upande mmoja endelea kufanya hivyo hadi vichanganyikane vizur baada ya hapo iache kwa saa 24.

2) Chukua kindoo kidogo na upunguze mafuta lita 3 kwa ajili ya kuweka rangi pembeni,weka rangi vijiko 3 ,changanya na mafuta uliyopunguza lita 3 kisha koroga mpaka yachanganyikane vizur kabisa.

3) Chukua coustic soda uliyoloweka kwenye ndoo kubwa ,kisha tia mafuta na uendelee kukoroga kuekekea upande mmoja kwa nguvu na kwa haraka,tia sodium silgett kwa kunyunyuzia kidogo kidogo, endelea kukoroga hadi vichanganyikane viwe kitu kimoja.

4) Baada ya hapo andaa ndoo nyingine ndogo ,chukuwa uji uliokoroga au mkorogo wako kias kwa ajili ya kuchanganya na rangi mwanzo na mafuta kisha koroga kwa pamoja vichanganyikane vizuri.

5) Kishaa andaa box la kukaushia sabuni na mimina mkorogo wako kwenye box ,kisha chukuwa mkorogo wenye rangi na umimine juu kwa stail ya zigzaga kisha pitisha mwiko ili rangi iingie mpaka chini.

Baada ya hapo iache kwa saa 24 ili ikauke vizur,kisha itoe na uikate kate sabuni yako.

Cha kuongezea kama unataka sabuni nyingi vipimo vinaongezeka,au kama ni kidogo vipimo vinapungua inategemea na ww mwenyewe unatakaje, nashauri nunua vipimo vidog kwa ajili ya kujifunza pale tu utakapo fanikiwa basi utaongeza kipimo kwa ajili ya kuuza.

Amka sasa wewe mama, kaka, dada, hii sio ya kukushindwa wewe usilalamike huna kazi wala biashara ya kufanya tembelea page zetu za @mwananchiscoop kujifunza zaidi kuhusiana na maswala ya biashara ili kuepukana na ujobless.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags