Mwanafunzi wa chuo auawa kwa risasi katika maandamano nchini Kenya

Mwanafunzi wa chuo auawa kwa risasi katika maandamano nchini Kenya

Mwanafunzi wa chuo kikuu aliyefahamika kwa jina la William Mayange amepigwa risasi shingoni na polisi, mjini Kisumu, katika maandamano dhidi ya serikali yaliyoandaliwa na viongozi wa chama cha Azimio La Umoja.

Inaelezwa kuwa mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu kutoka Chuo Kikuu cha “Maseno,”  alikuwa miongoni mwa wanafunzi walioandamana na kuvamia supermarket.

Aidha kwa mujibu wa ripoti ya polisi, waandamanaji waliwazidi nguvu polisi ambao waliishiwa mabomu ya machozi, ndipo risasi za moto zikarushwa ili kuwatawanya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags