MTAZAMO: Utatuzi wa afya ya akili kwa vijana unahitajika

MTAZAMO: Utatuzi wa afya ya akili kwa vijana unahitajika

Hivi karibuni limetokea wimbi kubwa kwa vijana kuwa na matatizo ya afya ya akili na hivyo kupelekea wengi kukatisha uhai wao na wengine hata kuua wenzao bila ya sababu.
 
Hali hii imekuwa ikitokea mara kwa mara na chanzo kubainika kuwa mapenzi, ukata na msongo wa mawazo ambao husababisha vifo vingi na majeruhi katika jamii.
 
Tatizo hili la afya ya akili huchangiwa na vijana kukosa taarifa sahihi, ushauri nasaha.
 
Kukosekana kwa mambo hayo huwafanya vijana wengi kufanya maamuzi yasiyo sahihi ikiwemo kujiua na hata kudhuru wengine.
 
Matatizo haya katika jamii yanaacha alama hasi kwani husababisha ongezeko la vifo, walemavu, yatima na sonona kwa badhii ya familia na watu husika kutokana na vifo visivyotegemewa na vya ghafla.
 
Wimbi la matatizo ya afya ya akili yamekithiri katika nchi hii ukizingatia wananchi wengi wanauelewa mdogo kuhusiana na afya ya akili na namna yakulinda afya zao kwa lishe, utamaduni na harakati za hapa na pale.
 
Hivyo wengi hufanya maamuzi bila kushirikisha mtu na baadae huleta athari katika jamii husika.
 
Tumezungumza na mtaalamu wa afya ya akili na uongozaji maisha Sumaiyya Mahmoud, ambae huchanganya tiba ya kitabia kwa uangalifu ili kukusaidia kutengeneza mabadiliko ya kudumu na kutoa fursa ya wewe kuleta matatizo yako, maumivu na hisia pasipo aibu wala kujutia. 
 
Changamoto za afya ya akili ni za utofauti kuliko huzuni ya hali au uchovu, ni makali zaidi na ya kudumu na yanaweza kuwa na matokeo mazito katika maisha ya kila siku. Moja ya changamoto za afya ya akili ni wasiwasi, huzuni, matatizo ya kula, matumizi ya madawa za kulevya na kupata Sonona.
 
Yanaweza kuathiri mfumo wa fikra kwa vijana, hisia au vitendo na kuingilia kwenye maisha ya kawaida.
 
Aidha, Serikali inapaswa kuangalia tatizo hili kwa jicho la tatu na kuhamasisha wanasaikolojia kuweza kutoa huduma kwa vijana na pia kuwezesha kuwapa uelewa  juu ya umuhimu wa kutambua afya zao za akili katika kufanya maamuzi ya maisha ya kila siku.
 
Hii itasaidia kupungua kwa maafa katika jamii na kuweza kuleta watu wenye mtazamo huru katika kufanya maamuzi ya kila siku na kuwezesha vijana kupata maarifa mapya ya namna yakuongoza maisha yao na kuangazia nyanja za maendeleo katika jamii.
 
Sanjari na hayo, vijana wengi wanakimbilia kupima maradhi mengine na kusahau kutambua afya zao za akili. Hili ni janga kubwa hivi sasa ambalo linatakiwa kutiliwa mkazo na hata pengine huduma hizi zipatikane shuleni, vyuoni hata vituo vya huduma rafiki kwa vijana. Hii itasaidia kukomboa vijana wengi.
 
Kuweza kudumisha taifa lenye nguvu kazi salama na kujitambua, afya ya akili itiliwe mkazo kama agenda nyingine ili kuleta manufaa katika jamii na hatimaye kupatikane kizazi kinachojitambua na kufanya watu wasiweze kuficha madhaifu yao kwa kuhofia kutokupata msaada, bali wawe wazi katika kuelezea changamoto zao na kupata suluhisho pasina kujidhuru wala kudhuru wengine. 
 
Hivyo basi wataalamu wa afya ya akili waungane na serikali katika kuboresha taifa hili na kuweza kudumisha umoja na amani.

Imeandaliwa na Shamsa khalfan,UDSM







Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags