Mr Ibu azikwa, fahamu zaidi kuhusu maisha yake

Mr Ibu azikwa, fahamu zaidi kuhusu maisha yake

Marehemu mwigizaji kutoka Nigeria John Okafor (62) maarufu Mr Ibu ambaye alifariki Machi 2, 2024 tayari amezikwa katika mji aliozaliwa wa #Amuri, Jimbo la #Enugu nchini humo.

Ikiwa zimetimia takribani siku 118 toka kufariki kwake, kaka mkubwa wa Mr Ibu, Sunday Okafor, alieleza sababu ya kuchelewesha mazishi hayo ni kwa ajili ya kumpatia maziko ya kihistoria mwigizaji huyo.

Mr Ibu alioa mara mbili na kufanikiwa kuwa na zaidi ya watoto 10 huku baadhi yao akiwaasili (watoto wa kuwalea) ambapo baadhi ya watoto hao ni Emmanuel Mandela Okafor, Chelsea Okafor, Jay Jay Okafor, Daniel Okafor, binti wa kulea Jasmine Chioma na wengineo.

Afya ya mwigizaji huyo ilianza kuzorota Oktoba 2023 wakati akijiandaa kurekodi filamu yake mpya na kupelekwa katika Hospitali ya Evercare huko Lagos, Nigeria ambapo ndipo alipofariki akiwa anapatiwa matibabu.

Mr Ibu alimaliza elimu ya msingi mwaka wa 1974 na kuahamia kwa kaka yake Sapele, katika Jimbo la Delta, Nigeria, baada ya kufiwa na baba yao mzazi.

Muigizaji huyo alimaliza elimu yake ya sekondari na kujiunga na Chuo cha Elimu kiitwacho Yola, kwa ajili ya kuendelea na masomo lakini hakuweza kumaliza kutokana na matatizo ya kifedha.

Aidha mkongwe huyo wa Nollywood jina lake lilianza kutambulika mwaka 2004 kupitia filamu yake ya ‘Mr Ibu’ ambapo alikuwa muhusika mkuu, akiendelea kujizoelea umaarufu kwenye filamu za akina Aki na Ukwa.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti mbalimbali nchini humo zanadai kuwa mpaka mauti yanamfika mkongwe huyo ameshaonekana katika filamu zaidi ya 200.

Sio uigizaji tuu pia mwigizaji huyo alijitoa kimaso maso katika muziki ambapo Oktoba 15, 2020 aliachia nyimbo mbili ambazo ni ‘This girl’ na ‘Do you know’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags