Mkuu wa polisi na afisa upelelezi wasimamishwa kazi

Mkuu wa polisi na afisa upelelezi wasimamishwa kazi

Taarifa kutoka mkoani  Morogoro ambapo uamuzi huo umefanywa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni dhidi ya Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD), SSP Shedrack Kigomanya na Ofisa Upelelezi Wilaya ya Kilombero, SP Daud Mshana

Aidha Sababu zilizotajwa ni malalamiko ya Wananchi kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na Viongozi hao ambapo Waziri Masauni amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP)  Camillus Wamburakuwachunguza na kuwahamisha maeneo yao ya Kazi

Hata hivyo kati ya malalamiko yaliyotajwa na Wananchi ni pamoja na baadhi ya Askari kuwakamata bila utaratibu, kunyimwa dhamana, kutozwa faini na madai ya kutumiwa na Wafanyabiashara wenye Fedha pamoja na kuwabambikizia Kesi za jinai

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags