Mchungaji atolewa WhatsApp kwa kufanya kolabo na mnenguaji

Mchungaji atolewa WhatsApp kwa kufanya kolabo na mnenguaji

Mwimbaji wa nyimbo za injili mkazi wa Eldoret nchini Kenya, Mchungaji William Getumbe amejikuta katika mgogoro na watumishi wenzake, huku wakimtoa kwenye kundi (group) lao la ‘WhatsApp’ baada ya kushirikiana na mwanamuziki Embarambamba anayepigwa vita kutokana na aina yake ya unenguaji.

Katika video ya TikTok, Getumbe ameelezea kusikitishwa kwake na kusema kwamba, wachungaji wenzake wamemuondoa kwenye makundi mbalimbali ya ‘WhatsApp’ kutokana na kushirikiana na Embarambamba katika wimbo wake mpya.

Hivi karibuni Embarambamba amekuwa akikabiliwa na shutuma za uvunjaji maadili kutokana na mtindo wake wa uchezaji wenye kunengua kwenye video zake za muziki.

Mhubiri huyo aliyevuma na wimbo wake mpya wa ‘Fuata Yesu’, ameonyesha kusikitishwa na wachungaji wenzakeo huku akiwashutumu kwa kumhukumu Embarambamba.

Kolabo yao ya hivi karibuni kati ya Embarambamba na Getumbe ilipokewa zaidi na mashabiki wa muziki ambapo Embarambamba ameonekana akiwa amevaa nguo ya marinda na Getumbe amevaa nepi kama sehemu ya kunogesha wimbo huo.

Katika mahojiano na mtandao wa TUKO, Getumbe alielezea kukerwa na tabia ya kuondolewa kundini, akihoji ni kwa nini wachungaji wenzake wanatupia lawama.

Getumbe anaamini kuwa wachungaji wanapaswa kumwachia Mungu hukumu badala ya kumtenga kutokana na kufanya kazi na Embarambamba.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags