Kajala, Harmonize yajayo yanafurahisha

Kajala, Harmonize yajayo yanafurahisha

UNAWEZA kusema yajayo yanafurahisha kuhusu kurudiana kwa mastaa wawili waliowahi kuwa ‘couple’ ya nguvu hapa Bongo, Harmonize na Kajala baada ya kila mmoja kufunguka kivyake juu ya kitendo hicho.

Baada ya kusambaa kwa video ya wawili hao wakikumbatia katika mashindano ya soka ya Samia Cup, stori zinadai wamerudiana japo Kajala anafanya kwa kujificha sana kwa sababu hapendi kumkera bintiye, Paula, anayesemekana hataki kusikia kuhusu uhusiano huo.

Mwanaspoti limepiga stori ya Kajala ambaye amesema kuwa yeye na Harmonize hawana ugomvi kwasasa kwani tofauti walishazimaliza kitambo.

“Kitendo cha kusalimiana ni moja ya ubinadamu, watu waniambie ni kosa kusalimiana? Halafu kitu kibaya sana ni kuweka kitu moyoni, kama watu walishatibuana huko nyuma na wakaja kuyamaliza sioni sababu ya kuendelea kuishi na chuki.

“Wanasema tumerudiana? Acha waongee wafikiriavyo, mimi hulka yangu sio mtu wa kufutalia mambo ya mitandao.”

“Sijali wanaongea nini maana nimeshaongelewa sana, nikifuatilia kila kinachoandikwa kuhusu mimi kwenye mitandao ya kijamii nitakuwa najikondesha tu, itanitesa na kunifanya nibaki mifupa mitupu bila sababu za msingi, hivyo sasa hivi siyapi nafasi kabisa mambo ya mitandaoni,” alisema Kajala.

Imekuwa kila wakati baadhi ya watu wengi wakiwahusisha wawili hawa kuwa, wamerudiana kisiri siri baada ya kuonekana au kuonyesha kwa watu kuwa hawana tofauti tangu watangaze kuachana mwaka 2022.

Mwaka jana Harmonize, alizungumzia taarifa hizo ambazo zimekuwa zikivuma kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa amerudiana na Kajala akisema hafurahishwi na kuhusishwa na mpenzi wake huyo wa zamani kuwa wamerudiana ilhali sio kweli na kusababisha kuharibika kwa uhusiano wake mpya.

Sasa mapya yamezuka baada ya video ya wiki iliyopita kuwaonyesha wakisalimiana kwa kukumbatiana huku watu waliokuwa karibu yao wakionekana kufurahishwa na kitendo hicho na kuimba kwa sauti ‘Konde Boy na Kajala.”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags