Mchungaji aliyefungisha ndoa ya Billnass na Nandy afunguka mazito

Mchungaji aliyefungisha ndoa ya Billnass na Nandy afunguka mazito

Moja kati ya taarifa ambayo imewaacha watu midomo wazi ni hii hapa inayohusisha maneno aliyoyazungumza Mchungaji aliyefungisha ndoa ya Billnass pamoja na Nandy katika kanisa la KKKT Mbezi beach, jijini Dar es salaam.

Akizungumza na maharusi hao mbele ya hadhara katika siku yao ya kufunga ndoa, aliwataka waumini kujitunza na kuhakikisha wanaingia kwenye ndoa takatifu ilihali wakiwa kwenye utakatifu.

“Kama msichana ni mjamzito na mtoto tumboni akiwa anasikia mnafunga ndoa ya watu wawili au mbona hamsemi nyie?”aliuliza swali hilo na akaongeza,

“Akiwa mtoto wa kike ni rafiki wa  baba, baba  akitembea naye mtamlaumu baada ya kuzaliwa?, akija mtoto wa kiume hapa mnkuja kuapa agano naye atakaposikia tumboni akaja akatembea na mama yake mtamlaumu? ni laana inapoanza,” alisema.

Alooooo! Haya wadau na wafuatiliaji wa Mwananchi Scoop una maneno gani ya kumwambia Mchungaji. Je unaunga hoja aliyozungumza mchungaji? Dondosha komenti yako hapo chini mtu wangu wa nguvu.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags