Mbinu za kufanikisha biashara ya vyakula mtandaoni

Mbinu za kufanikisha biashara ya vyakula mtandaoni

Mambo vipi? Unataka mkwanja wewe? Najua jibu “ndiyo!” kama kawaida mtu na michongo yangu, nakupa fumbo la mkwanja kazi kwako kufumbua kuzipata hizo pesa.

Basi bhana leo katika biashara tunaingia darasani kidogo kuboresha kile tulichonacho ili twende sawa na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Kama tunavyojua namna biashara zinavyoendeshwa siku hizi ni kidijitali basi wafanyabiashara nao inabidi kwenda sawa na kasi hiyo, basi nakupa fursa ya kuzifahamu mbinu ambazo mfanyabiashara anaweza kuzitumia katika kufanikisha biashara ya uuzaji chakula mtandaoni.

Twende pamoja darasani kujifunza mbinu hizo kama umepanga kutumia fursa hii ya uuzaji chakula mtandaoni na baadhi ya mbinu muhimu za kufuata wakati wa kuanzisha biashara ya vyakula mtandaoni ni pamoja na;-

  • Fahamu vyema na kuzifuata sheria za uuzaji wa vyakula mtandaoni.

Kabla hujafanya chochote, unahitaji kuhakikisha kuwa una uelewa wa

kanuni na sheria zinazomuongoza mfanyabiashara wa uuzaji wa vyakula mtandaoni. Mfano, ni muhimu kujiuliza Je, vyakula unavyotaka kuuza unaandaa kutoka nyumbani au una sehemu maalumu kama mgahawani? Ni wazi sheria utakazotakiwa kufuata zitakuwat ofauti na yule mwenye mgahawa. Hivyo kwa ujumla unatakiwa ujiandae kwa vitu kama:

  1. Ukaguzi wa mara kwa mara kutoka mamlaka ya chakula na dawa (TFDA)
  2. Kibali cha kuuza vyakula kutoka mamlaka ya TFDA
  • Leseni halali ya kufanya biashara
  1. Uwezo thabiti wa kuhifadhi vyakula katika hali ya usafi (Majokofu na makabati ya vyakula n.k)
  2. Hakuna wanyama (mbwa/paka) nyumbani au jikoni kwako

Hizi ni baadhi ya mwongozo wa sheria na kanuni muhimu za kufungua

biashara ya chakula unaopatikana TFDA ambapo utaweza kuzifahamu

kwa umakini kanuni zote kabla ya kuanza kuuza  chakula mtandaoni.

  • Chagua soko na aina ya vyakula

Kila mtu anakula lakini haimaanishi kila mtu anaweza kuwa mteja

wako kulingana na vyakula unavyopika na kuuza.

Mjasiriamali anatakiwa kujua aina ya wateja ambao ndio soko la bidhaa yake ya chakula, aina ya vyakula wanavyopenda,  hii itasaidia kurahisisha vitu kama pale utakapotaka kufanya marekebisho ili kukidhi haja za wateja wako.

Chagua aina ya chakula ambacho unaweza kukiandaa vizuri, Pili hakikisha unawatambua wateja wako kufuatana na bei unayouzia chakula Mfano, kama umeamua kuuza pilau au biriani kwa shilingi 20,000/= ni lazima ujue mteja wako atakuwa nani na atatoka wapi. Lakini ni muhimu pia kuchagua soko ambalo unaweza kulitawala licha ya kuwa na ushindani mkubwa kulingana na uandaaji wa bidhaa yako.

  • Tengeneza jina

Baada ya kuhakikisha unajua nini utakachouza na nani utamuuzia, basi

itakuwa rahisi sana kwako kutengeneza na kukuza jina lako. Mara

nyingi jina la kampuni au mjasirimali litakua na kujulikana kutegemeana na chakula

unachoouza. Pia muhimu kuhakikisha jina linasadifu unachofanya na utofauti na bidhaa zingine kutoka sehemu yeyote, lakini jina la biashara yako ni muhimu lieleze kwa nini waje kununua kwako.

 Mfano, kama unauza keki basi ifike mahali watu wakisema keki wanakuongelea wewe au wakisema biriani wanakutambua kuwa wewe ni bora zaidi. Kukuza jina kunaweza kupitia ubora wa chakula chako, huduma kwa wateja na kitu cha tofuati ambacho hakipo katika biashara nyingine. Kwa mfano katika mavazi ya watoa huduma, namna ya kuwafikia wateja wako kwa wakati na vifungashio (package) au bei ambazo itakuwa tofauti na wengine.

  • Vifungashio na lebo

Bidhaa inaweza kuuzika kwa haraka au wepesi kutokana na muonekano wake katika ufugaji (package). Mara nyingi wafanyabiashara wa vyakula vya mtandaoni huwa na vifungashio vya vyakula vizuri ili kumshawishi mteja ambacho ni kitu muhimu sana. Ukiachilia mbali kuambatanisha vitu kama jina la biashara/bidhaa rangi zinazoakisi biashara yako na nembo kuna vitu vingi inatakiwa uangalie wakati wa kufunga vyakula vyako. 

Vyakula vinatakiwa vifungwe katika hali ya usafi wa hali ya juu kama

ni chakula ambacho kinahitaji kuhifadhiwa kwenye sehemu yenye

ubaridi basi kifungashio chake lazima kiakisi hilo na kama ni vyakula

ambavyo haviharibiki kwa haraka, mfano asali basi hakikisha pia

vifungashio vyake vina ubora wa kutosha.

 Kuna sheria na kanuni za kufunga na kutunza vyakula, hivyo ni muhimu kuzingatia kanuni zinazotakiwa kufuatwa wakati wa kuweka lebo katika vifungashio, mfano:

  1. Orodha ya viungo vilivyomo
  2. Kiwango/uzito
  • Jina na sehemu ilipo kampuni
  1. Tarehe ya mwisho wa matumizi n.k

Ni muhimu kuhakikisha unatimiza mahitaji ya sheria ili kuepuka

usumbufu wakati unaanza kutangaza na kusambaza vyakula vyako

mtandaoni.

Mfanyabiashara anatakiwa kuwa mbunifu katika aina yake ya ufungaji wa bidhaa yake kama unauza asali au chakula basi tafuta kifungashio ambacho kiko tofauti na vingine ili wateja waje kwako.

  • Tangaza chakula chako

Hii itakusaidia kutengeneza uhusiano na wateja wako ambapo ni nguzo muhimu ya biashsara ya mtandaoni ili Kuitafutia bidhaa yako masoko na kuitangaza, Kuna njia nyingi sana za kutangaza na kufanyia masoko biashra yako ya chakula.

Unaweza kutangaza kupitia kurasa za mitandao ya kijamii, mfano zitakusaidia kutengeneza uhusiano kati yako na wateja wako. Si unajua maoni yao (hasi na chanya) ndio kufanikiwa kwa biashara yako?

 Hivyo, bila hivi huwezi kujua watu wanapenda au hawapendi wanaongea nini kuhusu bidhaa yako.

Pia usisite kushiriki katika makongamano ya vyakula ambapo watu

tofauti hualikwa kuonja ladha tofauti za vyakula zinazouzwa na wauzaji

tofauti hivyo unatakiwa kubeba kadi za biashara (business cards) na kuwa tayari kutoa ofa, mfano kupeleka chakula sehemuyeyote bure kwa wateja wapya.

Hizo ndo baadhi ya mbinu ambazo wadau wa uuzaji chakula mtandaoni wameshare na Mwananchi Scoop katika kona ya biashara ili kuongeza thamani kwa mfanyabiashara na kuweza kukua kwa kutanua soko la uuzaji chakula,kwa story hizi na zingine nyingi kuhusiana na biashara utazipata kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii.

Unataka kujua wiki ijayo kwenye biashara tutakuletea nini? Kaa chonjo!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post