Mastaa wanaotupia zaidi mwezi huu

Mastaa wanaotupia zaidi mwezi huu

Hellow! Watu wangu wa nguvu kama kawaida yetu kwenye magazine yetu kuna segment mbalimbali ambazo zinakufanya uburudike na kuenjoy. Basi week hii katika kile kipengele chenu pendwa cha fashion tunakusogezea baadhi ya mastaa ambao wanajua kutupia sana.

Kama wewe unapenda kuvaa basi ungana nami kujua baadhi ya mastaa ambao wametupia na kutokelezea. Kama unavyojua kuna mastaa wanajua kuvaa bwana, yaani wao kila week, kila siku ni full ng’aring’ari, wenyewe wanakwambia hawana Jumamosi wala Jumapili, wao ni kupendeza tu. Waswahili wanasema ukitaka kuwa mrembo au kupendeza basi usiwe mbahili bibi weee, hahaha.

  1. MALIKA DESIGNER

Wa kwanza kabisa ni mwanadada makini sana ambae yeye ni mjasiliamali Malika Rashid maarufu kama Malika Designer, yeye hujishuhurisha zaidi na kudesign nguo za kume na za kike, basi bwana mwanadada ambae anajua kuchagua rangi inayompendeza na kujipangilia uzuri kabisa kuanzia juu hadi chini.

Si hiayo tuu mwanadada huyu katika maswala ya mpangilio wa mwonekano wake hana mchezo kabisa, alizua taharuki kwa jinsi alivyo tokelezea katika “usiku wa raha za pwani,” ambapo wengi wao waliofika eneo la tukio na waliofanikiwa kuangalia katika television (TV) zao, kila mmoja alikubali mwonekano wake, bwana weeeeh! Anaenuna na anune mimi nasema yeye ndo alipendeza ukumbi mzima ukibisha niite mbwa nimekaa pale.

  1. HAMISA MOBETTO

Alooooh! Nisipo mtaja mrembo huyu nitakuwa nimewakosea sana. Wa pili katika chat yangu ni Hamisa Mobetto. Huyu binti bwana anavaa, sio kuvaa tuu, yaani anavaa na nguo inakaa mahali pake. Kwanza anajua

kujipangilia kuanzia juu mpaka chini, halafu waswahili wenzangu sio kuvaa na kuwa na mwonekano mzui wa nguo, je una damu ya nguo? Hili nalo ni tatizo haswaaa!

Kama tunavyojua kuwa Hamisa ni designer ambae mara nyingi sana hujivalisha mwenyewe, mwanadada huyu bwana ni kipenzi cha wengi kutokana na jinsi anavyojua kujipangilia katika mavazi, katika mastaa ambao ametupia zaidi kwenye top 5 huwezi kumkosa mwanadada huyu, hata ukifuatilia katika mitandao yake ya kijamii utaelewa nini nazungumzia na hii ni sababu ya wewe msomaji wangu kama unataka kupendeza basi angalia nini mwanadada huyu anafanya.

  1. WEMA SEPETU

Karata yangu ya tatu bwana inakwenda kwa ‘Madame’ mwenyewe kabisa. Waswahili wana kamsemo kao kuwa “amegoma kuzeeka.” Uongo dhambi bwana, nae yuko vizuri haswa katika kujipangilia mavazi yake kuanzia rangi mwonekano na mpangilio wake kuanzia juu mpaka chini.

Kwa miezi ya hivi karibuni madam Wema ameonekana kutupia haswa akipata mualiko katika shughuli za watu mbalimbali, kwa warembo mastaa wanaojua kutupia usipo mtaja mwanadada huyu ni kama umemuonea, yaani anajua nikivaa hivi nitapendeza na niukivaa hivi nitatisha.

  1. AUNTY EZEKIEL

Uwiiiiih! Mambo yanazidi kunoga bwana maana mastaa kiufupi mwaka huu wameamua haswaa basi bwana bila ya kumsahau mama ake na Noman, Aunty Ezekiel, nae ana balaa huyo, yaani ni kama sio mama wa watoto wawili.

Ukitaka kumjua huyu mrembo anajua kupendeza, anajua kutupia, basi angalia pale anapopata mualiko katika sherehe fulani yaweza kuwa harusi au jambo lolote lile, ndo utaelewa nini namaanisha, mama Nonoh bwana japo kuna maneno yanavuma kupitia mitandao ya kijamii kuwa ameongeza shepu lakini na kuvaa pia anajua bwana weeeeh!.

  1. QUEEN DARLEEN

Nyie nyie sijui niseme au ninyamaze ila wacha nilimwage bwana. Hivi wafuatiliaji wa Mwananchi Scoop mnaonaje mwonekano wa dada ake msanii mkubwa nchini Diamond, Queen Darleen? Uongo dhambi nyie, huyu dada nae siku hizi anajua kutupia bwana anapendeza, kama unabisha wala hatukulazimishi ila ukweli ndo huo.

Baadhi ya watu walikuwa wanamuona wa ajabu kwa kujiweka kama mwanaume lakini sasa hivi toka apate mtoto anatupia haswa na anapendeza mno. Hivyo basi ndo maana tukamuweka katika listi ya mastaa ambao wametupia na kupendeza zaidi katika mwezi huu na mwezi uliopita.

Najua kuna mastaa wengi ambao wanapendeza wanatupia lakini kwa week hii tufanye kama tumemaliza, sitaki kuwachosha sanaa. Ushauri tuu, kama unahitaji kuwa na muonekano mzuri inabidi ujue kujipangilia kuanzia juu mpaka chini ikiwezekana tafuta designer ambae atakuwa anaelewa mwili wako unaendana na mavazi gani, usikurupuke tuu kwa kumuona Mobetto au Malaika kapendeza ukajua na wewe utapendeza, cha kuzingatia ni kujua kujipangilia.

Oooooooohoooh! Bwana bwana naona kwa week hii tuishie hapa watu wangu wa nguvu, usikose kufuatilia fashion ya next week kama kawaida yangu nawashushia vigongo tuu vile moyo unapenda. Usisahau kufuatilia mitandayo yetu ya kijamii @Mwananchiscoop.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags