Sababu Tom Holland Kutoongozana Na Mpenzi Wake

Sababu Tom Holland Kutoongozana Na Mpenzi Wake

Mwigizaji maarufu ambaye amefanya vizuri kupitia filamu ya Spider Man, Tom Holland amefunguka sababu ya kutoongozana na mpenzi wake Zendaya kwenye red carpets wakati wa uzinduzi wa filamu kwa kudai kuwa akiwa naye karibu anapoteza umakini.

Tom ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye mahojiano na Men’s Health siku ya jana Alhamisi Januari 2, 2025 ambapo alidai kuwa hawezi kuongozana naye kwa sababu sio wakati wake.

“Kwa sababu si wakati wangu, ni wakati wake, na tukifika pamoja, inakuwa kuhusu sisi, nikiwa naye karibu na kumtizana napoteza umakini wa sehemu husika” amesema Holland

Kwa mujibu wa Page Six, Holland hakuonekana kwenye zulia jekundu wakati wa uzinduzi wa filamu ya mpenzi wake Zendaya, iitwayo Dune: Part Two na Challengers inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.

Wanandoa hao, ambao walithibitisha uhusiano wao rasmi mwaka 2021 wanatarajiwa kuonekana tena pamoja kwenye filamu yao ya nne ya Spider-Man, inayotarajiwa kutoka mwaka 2026.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags