Ili Uoe Unatakiwa Ukate Mikono Na Umpe Mke Kama Mahari

Ili Uoe Unatakiwa Ukate Mikono Na Umpe Mke Kama Mahari


Kama unajidanganya kuwa umeshawahi kuona kila kitu kwenye dunia hii basi nakujuza kuwa bado kunavitu haujawahi kuviona kabisa.

Kibongo bongo baadhi ya vijana wanagoma kuoa huku sababu yao kubwa ikiwa ni wingi wa mahari wanayotajiwa, lakini hii ni tofauti kabisa katika moja ya kijiji kilichopo Vietnam ambapo wanaume wanalazimika kukata mikono na kumpatia mwanamke atakaye muoa kama zawadi ya mahari.

Kufuatia na video inayoendelea kusambaa mitandaoni imeonesha asilimia kubwa ya wanaume waliopo katika kijiji hicho hawana mikono jambo ambalo liliwashitua wengi katika mitandao ya kijamii huku wengi wao wakidai kuwa ni bura kuwa single milele.

Aidha kwa mujibu wa baadhi ya wanaume hao wameweka wazi kuwa kumkabidhi mke mtarajiwa mikono kunamfanya mwanamke huyo kuwa na furaha na kujiamini kama anapendwa kweli.

Mbali na watu hao kukatwa mikono lakini wanaonekana kuzoea hali hiyo huku wengi wao wakiendelea na majukumu yao ya kila siku kama vile kuchora, kupiga piano na mengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags