Makabila Ajutia Kumpa Talaka Zaiylissa

Makabila Ajutia Kumpa Talaka Zaiylissa

Mwanamuziki wa Singeli hapa nchini, Dulla Makabila ameweka wazi kuwa anajutia kumpa talaka aliyekuwa mke wake, Zaiylissa.

Makabila amefunguka hayo leo Januari 3, 2025 kwenye mahojiano yake na Clouds FM.

“Ndio najutia, nakumbuka nilitoa tatu, yaani talaka naweza kusema ni kitu kibaya sana hata katika ndoa yangu ya kwanza, mimi kitu ambacho kinanifelisha huwa nina hasira sana na maamuzi ya hasira yanakuwa sio mazuri hata kidogo.

"Unafanya maamuzi halafu baadaye unakaa peke yako unaona daah! Hii si sawa kwa sababu baada ya hii ishu kutokea ndio nikajua mapenzi yalivyo.

"Unaweza kuwa na kila kitu, unapata hela, unapata shoo, una magari mawili mawili lakini unakaa unaona kabisa kuna kitu hakipo sawa,” amesema Dulla Makabila.

Mbali na hilo, mwanamuziki huyo aliweka wazi kuwa bado anampenda Zaiylissa na huwa akipostiwa na mume wake wa sasa ambaye ni Haji Manara huwa anaumia sana.

Mei 2023, Dulla Makabila alifunga ndoa na Zaiylissa na kudumu katika ndoa hiyo kwa takribani miezi mitatu. Baada ya kuachana mwanadada huyo aliolewa na aliyekuwa msemaji wa Yanga, Haji Manara.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags