Jarida maarufu Duniani 'Wealth' linalojihusisha na kutoa ripoti mbalimbali kuhusu utajiri na umiliki wa mali kwa watu maarufu duniani. Limetoa orodha ya watu maarufu wanaopokea pesa nyingi zaidi kupitia matangazo ya Instagram.
Katika orodha namba moja inashikiliwa na Christiano Ronaldo ambaye ana wafuasi milioni 651 Instagram yeye anatoza Dola 3.23 milioni huku nafasi ya pili ikiendea kwa Lionel Messi ambaye ana wafuasi Milioni 505 kwenye mtandao huo analipwa dola 2.59 milioni kwa tangazo moja.
Selena Gomez, ambaye ni mwigizaji na muimbaji kutokea Marekani ambaye ana wafuasi zaidi ya milioni 421 yeye hukusanya kiasi cha dola 2.55 milioni kwa post moja ya tangazo kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Kylie Jenner, ana wafuasi milioni 421 Instagram hutoza kiasi cha dola za kimarekani 2.38 milioni kwa ajili ya post moja ambayo inaweza kuwa ya tangazo au kampeni mbalimbali
Dwayne Johson, maarufu kama The Rock ambaye ni mwigizaji tokea Marekani yeye ana wafuasi milioni 394 kwenye ukurasa wake wa Instagram na hutoza dola 2.32 milioni kwa post moja ya tangazo kwenye ukurasa huo.
Ariana Grande, ambaye ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo na mwigizaji kutokea nchini Marekani ana wafuasi milioni 376 Instagram na anahitaji dola 2.26 milioni kwa ajili ya tangazo moja kwenye ukurasa wake.
Kim Kardashian, yeye ana wafuasi milioni 357 kwenye ukurasa wake wa Instagram na anatoza dola 2.17 milioni kwa tangazo lolote kutokea kwenye ukurasa wake huo.
Beyonce, ambaye ni mwanamuziki nguli kutokea nchini Marekani ambaye amejizolea umaarufu kutokana na uwezo wake wa kuimba anawafuasi milioni 312 yeye hutoza dola 1.89 milioni kwa ajili ya post moja ya tangazo kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Khloe Kardashian ambaye ni ndugu wa damu wa Kim kardashian anajumla ya wafuasi milioni 303 kwenye ukurasa wa Instagram na hutoza dola milioni 1.87 kwa ajili ya post moja ya tangazo kwenye ukurasa wake.
Justin Bieber, mwimbaji tokea nchini Marekani ambaye ana jumla ya wafuasi milioni 294 kwenye ukurasa wake wa Instagram hutoza kiasi cha dola za kimarekani 1.76 milioni kwa kila post moja ya tangazo au kampeni fulani kwenye ukurasa wake.

Leave a Reply