Mastaa waliojitokeza kwenye tamasha la Michael Rubin

Mastaa waliojitokeza kwenye tamasha la Michael Rubin

Mastaa katika Nyanja mbalimbali wamejitokeaza katika tamasha linalofanyika kila mwaka ambalo linaandaliwa na mfanyabiashara mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Fanatics, jukwaa la kimataifa la michezo ya kidijitali Michael Gary Rubin.

Mastaa ambao wameonekana katika tamasha hilo lililofanyika katika eneo lake la ufukwe ‘Hamptons estate’ ni kama Kim Kardashian, Drake, Jay-Z, Lil Wyne, Jake Paul, Wiz Khalifa, Travis Scott, Meek Mill huku baadhi ya mastaa wa soka akiwemo Asharaf Hakimi na wengineo.

Michael Gary Rubin ‘White Party’ inafanyika kila mwaka ikiwa ni msimu wa nne sasa imeripotiwa kuwa bilionea huyo anaamua kufanya party hiyo na kualika watu mashughuli kwa lengo la kuwaweka mastaa hapo pamoja ili waweze kubadilishana mawazo.



Aidha kwa mujibu wa mke wa bilionea huyo aitwaye Camille Fishel ametolea ufafauzi party hiyo kwa kudai kuwa ilikuwa ni bora zaidi kushinda za miaka yote ya nyuma.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post