Zikiwa zimebaki wiki kadhaa kuupindua mwaka 2024 na kuingia 2025, mtandao wa kuuza na kusikiliza muziki wa Spotify umeshusha orodha ya wasanii wanaosikilizwa zaidi kutoka Tanzania.
Mapema leo Desemba 5, 2025 Spotify imetaja kuwa kati ya wasanii 10 waliosikilizwa sana Tanzania, wanne ni wasanii wa Tanzania na 6 (sita) kutoka nchi nyingine Barani Afrika.
Kati ya wasanii hao ni pamoja na Marioo, Diamond Platnumz, na Harmonize. Huku Alikiba akishika nafasi ya 10.
Aidha mbali na hilo pia mtandao huyo umeorodhesha album zilizosikilizwa zaidi ni pamoja na “The Kid You Know” – Marioo, “Visit Bongo”- Harmonize, “Therapy”- Jay Melody, “Most People Want This”- Navy Kenzo, na “Made For Us” yake Harmonize.
Hata hivyo kupitia orodha hiyo imeonesha nyimbo 10 zilizosikilizwa ndani ya Tanzania na Afrika kote huku orodha hiyo ikiongozwa na wimbo wa Hakuna Matata wa Marioo.
Nyimbo nyingine ambazo zimesikilizwa zaidi ni pamoja na “Mapoz (ukiwashirikisha Mr Blue & Jay Melody)” – Diamond Platnumz, na “Buruda” – Jaivah, : “Zawadi (Dadiposlim) – Zuchu, “Dharau” – Ibrah, na “Nisiulizwe” – Jux. Huku wasanii waliosikilizwa sana ni Marioo, Diamond Platnumz, Jay Melody, na Jaivah.
Leave a Reply