Makosa ambayo hutakiwi kabisa kuyafanya ukiwa chuoni.

Makosa ambayo hutakiwi kabisa kuyafanya ukiwa chuoni.

Niaje niaje wanangu wa vyuoni najua sijachelewa sana kuwaeleza kuhusiana na majambo haya, na hata kama umechelewa unaweza kuyarekebisha coz I hope muda utakuwa nao wa kuyarekebisha hayo.

Mada yaleo ni fupi lakini ukiisoma na kuielewa basi utakuwa umepiga hatua kubwa sana, kuna baadhi ya marafiki zangu niliomaliza nao chuo huyajutia sana haya makossa, nimekuja na ujumbe huu kwasababu tuu nawewe usije ukaingia katika mkumbo huo.

Mmmmh! Sijui hata nianze na lipi, maana, haya hapa baadhi ya makosa ambayo hutakiwi kabisa kuyafanya ukiwa chuoni.

  1. Kutokusave hela ya boom

Kuna baadhi ya wanachuo wakishapata pesa ya boom basi wanasahau kabisa kama atakuja atamaliza chuo na hatakuwa na kazi ya kufanya wala biashara, lakini ukitumia boom lako vizuri katika kuwekeza hata kama kwenye biashara ndogo badae itakuja kukusaidia utakapo maliza, kama tunavyojua siku hizi ajira ngumu watu wengu hutumia pesa zao za boom kwa kutengeneza maisha yake ya badae.

So jitahidi sana kusave pesa utakayo tumiwa na wazazi wako na pesa yako ya boom itakuja kukusaidia hapo baadae.

  1. Kupoteza muda kwenye mahusiano

Kiukweli mahusiano mengi ya chuo hayadumu, na yanayo dumu ni mmoja kwa kumi, Ila hilo halina maana yote, wengine hudumu. Utajikuta unachezewa na kila mwanaume na kuachwa kwa sababu tuu yakuambiwa kuwa usipokuwa na mahusiano chuo utaonekana mshamba.

Usipoteze muda wako kwa vitu vya mpito, haujakatazwa kuwa na mahusiano lakini angalia na mtu wa kuwa na mahusiano nae sio unabeba beba tuu utakuja kubeba visivyobebwa.

  1. Kutokujali na kuweka effort sana kwenye masomo

Kuna baadhi ya marafiki zangu niliosoma nao walikuwa hawaingii katika vipindi na walikuwa hawajali nini kilicho waleta chuo, baadhi yao ukiwauliza unasoma unataka kuwa nani atakacho kujibu nasoma kwasababu wazazi wangu wametaka nisome na wengine ni kwasababu tuu waliambiwa chuo bata usome utafaulu na usisome utafaulu, lakini hii imekuja kuwaletea mazara makubwa ya kurudia semester nk.

Matokeo yako yote yanaumuhimu kuanzia semester ya kwanza hadi ya mwisho ya mwaka wa tatu, zingatia sana hili utakuja nishukuru badae na ukiamua kulipuuzia basi utakuja kuelewa nini namaanisha hapo utakapo maliza na kuwa na cheti chako mkononi.

  1. Kudoji darasani

Kwanza mimi kichwa change nakijua mwenyewe nisipo ingia darasani basi hiyo sehemu waliofundishwa wenzangu sitokuja kuielewa hata anielekeze nani labda lecture arudie tena, yaani sikushauri kabisa ukafanya kosa hili la kudoji na hili sio mimi baadhi yetu wengi tuko hivi, na hili swala linaweza kukukosti ukapata hata kesi chuoni kama uko na udhuru basi toa taarifa.

Hili kosa linaweza kukukosesha hadi maksi chuoni, kuna baadhi ya malecture wanaamka na moods zao anaweza kuingia class nakusema anatoa quiz au test utakuwa umeshakosa maksi ambazo ungefika hata kama hukusoma ungeambulia hata 10.

Haya sasa ndio  makosa machache kati ya mengi ambayo nimeyashuhudia nikiwa chuo, ambayo sitamani na wewe ndugu yangu ulioko chuoni uweze kuyapitia.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags