MAHUSIANO: Wanawake kuwa tegemezi ni kujiendekeza

MAHUSIANO: Wanawake kuwa tegemezi ni kujiendekeza

Kuna jambo nimekuwa nikijiuliza maswali nikawa nakosa majibu lakini nilipojaribu kufanya utafiti mdogo nimegundua sababu kadhaa zinazosababisha janga hili linalowaathiri watoto wetu wa kike. Nadhani tunapaswa kama wazazi tuwafundishe watoto wetu wa kike kujitegemea na kujiamini kama binadamu waliokamilika.

Hili siyo suala la kusubiri wafundishwe shuleni au kusubiri wajifunze kupitia mitandao ya kijamii. Kuna hatari kubwa kuwaacha mabinti zetu kutegemea watu maarufu mitandaoni kuwa ndiyo roll model wao ni kosa kubwa.

Naomba niwape mifano kadhaa...

Kwa mfano kuna namna nyingi ya watu kukutana na kujenga ukaribu kati ya wanawake na wanaume. Ipo mitandao ya kijamii, Makundi sogozi, michapalo, hafla mbalimbali, makazini na kwenye makongamano ya imani, mashuleni, vyuoni na kwenye shughuli za kijamii...

Huko watu yaani wanawake na wanaume wanaweza kubadilishana namba za simu na kujenga ukaribu kwa kuwasiliana mara kwa mara. Shida inaanza pale mwanaume anapojenga ukaribu na mwanamke kabla hata ya kuonyesha kuomba kuwa na uhusiano wa kimapenzi linakuja bomu la kuombwa hela. Lakini kabla ya kufikia hatua hiyo mwanamke ataanza kujenga mazingira kwa kutumia majina ya Dear, my love, darling, sweetheart, baby....nk.

Kabla huajua kinachoendelea....

Linakuja Boom....

"Baby leo sijapata lunch..."

Au "baby sina nauli"

Au nikopeshe hela ya kodi nk...

Hii tabia naishuhudia kwa wadada wengi tena wengine wenye kazi zao nzuri tu. Hizi kelele zinazopigwa na wanaume mitandaoni kulaumu hizi tabia siyo za kupuuza. Wanawake tumieni majukwaa yenu kujitafakari. Inawezekana mwanaume ana nia nzuri   na mwanamke lakini akishaona viashiria hivi anasepa mapema. Hakuna mwanaume anayependa mwanamke Kupe. Labda itokee amempenda mwanamke kweli kweli lakini mwingine anaweza kukubali kuwa mtumwa wa kuombwa hela lakini akisha mega anasepa. Hapo ndipo mwanamke ataona analogwa kwa sababu kila mwanaume anamega na kukimbia...

Ni kitu gani kinatawala vichwa vya wanawake hawa...?

Nadhani zipo sababu nyingi zinazowafanya dada zetu nyingi zikiwa zimejengwa na wanaume  wenyewe... Kitu cha kwanza ni ule upendeleo wanaopewa wanawake katika maeneo mengi.

Kwa utafiti wangu mdogo nilioufanya katika mazingira yangu ya kazi nimegundua kwamba baadhi ya wasichana wanachukulia kama kile kitendo cha kuzaliwa mwanamke tayari ni fursa. Yaani kuna kitu kwenye akili yao ya kina (subconscious mind) kinawaambia thamani yao iko kwenye uanawake wao. Ndiyo maana ukimuomba mwanamke mtoko (date) ataifungamanisha na kutongozwa.

Hata mwanaume kumsaidia tu mwanamke katika hali ya kawaida anaweza akadhani anatakwa kimapenzi jambo ambalo inawezekana lisiwe ni lengo la mwanaume kutoa msaada. Mwanamke anatanguliza utupu wake kama rasilimali ya kupata huduma tena pengine nyingine ni halali yake na wanaume wamegundua hilo nao wamegeuka kuwa wateja na wanawake wakiwa ni wauzaji.

Wanaume wengi huwaheshimu wanawake wenye misimamo na wanaojitegemea kuliko wale wanaotarajia kupokea. Mwanamke ombaomba anajidhalilisha bila kujua na ndiyo maana wanaume huwa wanapasiana tu kila mtu ajilie kwa nafasi yake.

Mwanaume anaweza kuchukua namba ya wanamke nap engine kuomba kutoka naye kiurafiki lakini matokeo yake ndani ya siku mbili anaombwa hela. Mwanaume anabaki anajiuliza anatoa pesa yake kwa makubaliano gani? Iwapo mwanaume ni muungwana atakataa kisiasa lakini kwa bahati mbaya wanawake hawa hawaelewi wataomba tena na tena.

Wapo mabinti nawajua wanaofanya kazi na hata kiwango cha mishahara yao nakijua lakini utakuta wanacheza upatu (Mchezo wa kupeana pesa), Kuna kikoba  na bado ana saccos na ukikutana naye atakwambia kaka naomba nauli nimeishiwa.

Unaweza kushangaa tumeombwa wanaume watano achilia mbali wale wa kwenye magrupu sogozi (Whattsup). Siyasemi haya kuwananga wanawake msinielewe vibaya, bali ningependa kuona wanabadilika.

Yupo Binti mmoja wa Kichina aliwahi kuniambia kwamba kule kwao nchini China ukimtongoza mwanamke na kuanza uhusiano anakataa kumnunulia vitu vya gharama na mara nyingi mkitoka out mnachangia kulipa bili.

Kwa nini?

Wenyewe wanasema hawataki uwagharamie ili wawe huru siku wakiona uhusiano wenu hauna mashiko wakivunja uhusiano mwanaume asiumie kwa gharama alizotumia kwa mwanamke huyo. Hapa kwetu ni tofauti. Mwanamke atahamishia shida zote za ukoo kwa mwanaume huyo utadhani kaoa ukoo...

Ninachojaribu kusema hapa ni kuwaomba wazazi kuwalea mabinti zao kiutambuzi wajitambue kuwa hata wao ni binadamu kamili na wanaweza kujitegemea bila kutegemea wanaume. Kwamba wana uwezo wa kutafuta fedha na kuishi maisha wanayotaka.

Uwanawake wao siyo kitega uchumi ni maumbile waliyopewa ili kupata watoto.  Kama ni starehe ifanyike kama takwa la kanuni ya maumbile siyo kutafuta fedha. Wanaume pamoja na tendo la ndoa lakini kuna vitu vingi wanaangalia kwa mwanamke. Kama huna sifa nyingine zaidi ya kutegemea utupu wanaume watakuwa wanapita tu na kusonga mbele.

Kama ni tendo la ndoa mwanaume anaweza kulipata kwa kununua barabarani maana wapo waliojiajiri kwa kutegemea via vyao vya uzazi. Hawa hawahitaji kuolewa wameona kuna hitaji hilo hususan kwa wanaume wasiojua kutongoza wakaona ni fursa kuwarahisishia.

Hawa hawahitaji kufikishwa kileleni wala maumbile makubwa, wanachojua ni kumridhisha mwanaume kwa makubaliano na mwanaume akimaliza shida yake wanamalizana. Sasa dada zetu ukiwaalika kwa mtoko utaombwa hela ya salon, kivazi na hela ya Uber na kwenye tendo lazima umfikishe kileleni na kama una maumbile madogo, subiri mkosane dunia yote itajua maumbile yako.

Haya hayawezi kufanywa na hawa wanaotoa huduma hiyo kwa malipo. Naomba mniwie radhi lakini naamini kuna cha kujifunza hapa.  Binafsi najisikia vizuri kumgharamia mwanamke nimpendae kwa hiyari yangu kiroho safi kuliko kuombwa ombwa hela. Lakini tukumbuke mahusiano hujengwa na mahaba ya kulipiziana.

Mwanaume akiwa mtoaji mwanamke anatakiwa ajiongeze kwenye maeneo mengine zaidi ya kutegemea uanawake wake pekee. Kwa mfano mwanaume akitoa hela ya shopping kwa mwanamke halafu mwanamke akajinunulia vitu vyake lakini akakumbuka kumnunulia mwanaume boxer jambo hilo litamvutia  sana mwanaume na kumthamini mwanamke huyo n ahata kumuweka kwenye nafasi nzuri ya kufunga naye ndoa. Kwa kawaida wanaume huivutiwa na vitu vidogo vidogo kutoka kwa wanawake na siyo kufanya mapenzi tu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Shaban Kaluse

A Sales and Marketing in the hospitality Industry and also a freelance journalist, writing about love and relationships and educative articles which aims for youths, every Tuesday on Mwananchi Scoop.


Latest Post

Latest Tags