Scene Za Mapenzi Zinavyomtesa Abdulrazak

Scene Za Mapenzi Zinavyomtesa Abdulrazak

Miongoni mwa waigizaji wapya wanaotikisa kiwanda cha filamu nchini ni Abdulrazak ambaye anaonekana kwenye tamthilia ya Jua Kali.

Licha ya kuonekana kwa mara ya kwanza akiigiza katika tamhilia hiyo, amejikuta akijizolea mashabiki wapya kila kukicha kutokana na kipaji chake cha kushangaza.

Akizungumza na Mwananchi Scoop mwigizaji huyo amesema safari yake ya kuigiza ilianza kama utani baada ya muongozaji wa tamthilia ya Juakali Lamata kumtafuta na kumuomba kufanya naye kazi.

"Kipaji hakijifichi nafikiri wenye macho waliona, Lamata aliona kipaji changu akanambia anahisi naweza kufanya vizuri kupitia tamthilia ya Juakali baada ya hapo tukakaa chini tukazungumza akanipatia muongozo wa stori nikaangalia nikasema acha nijaribu kufanya," amesema Abdulrazak.

Mapokezi ya watazamaji wa Tamthilia hiyo kwa Abdul ambaye anacheza kama Davis yamekuwa makubwa anasema anaona kuna deni anahitajika alilipe kwa ajili ya tasnia ya filamu nchini.

"Watazamaji ndio wanatupa picha kuwa tunafanya kazi nzuri au mbaya, mapokezi niliyopewa na mashabiki sikuwahi kuyaona wala kuwaza nathubutu kusema Tanzania kwa sasa imenipa deni la kuifikisha hii tasnia kimataifa," amesema Abdul .
Hata hivyo amesema matamanio yake mpaka sasa ni kuongeza juhudi siku moja itajwe kwenye Tasnia ya Filamu Kimataifa.

"Kabla sijaingia kwenye sanaa nilikuwa mtu wa kutoa motisha kwenye mapenzi na mahusiano mfano namna gani kumtuliza mwanamke n.k na mpaka sasa sina mpinzani kwenye engo hiyo.

Kwa hiyo hata wale waongozaji na watayarishaji waliona hiyo rasilimali kwangu na ndiyo maana wananipa sini za namna hiyo na kweli maudhui ya namna hiyo nafanya vizuri na mashabiki wangu wanayapokea kwa ukubwa sana" amesema

Ameongeza kuwa licha ya kufanya vizuri kwenye sekta hiyo ya mahusiano bado anapitia changamoto kwani kuna muda anahitajika kufanya vitu ambavyo kwa watu wake waliomzoea kama shekh na mtu wa dini inakuwa ngumu kumuelewa.

Utakumbuka kabla ya kuingia kwenye uingizaji wengi walimfahamu kama Shekh ambaye anatibu kupitia dua lakini mtoa ushauri wa mahusiano, kwa sasa anatamani watu wamfahamu kama mwigizaji.

"Kwa sasa hivi Tanzania na Duniani naomba niitwe mwigizaji iwe namba moja ndiyo ifuate mtu wa motisha," amesema Abdul.

Amesema licha ya kuingia kwenye uigizaji haimfanyi kutoshiriki kwenye shuguli zake ambazo alikuwa akizifanya hapo awali.
"Ninapokuwa off utanikuta ofisini kwangu naendelea na shughuli zinazonihusu lakini nikiwa kwenye kuandaa filamu nakuwa huko tu kwahiyo bado naendelea. Hakuna kilichobadilika kila kitu kinaenda sawa,”amesema

Ameongezea kwake ni heshima kubwa kuona anatafutwa na watayarishaji wa filamu wakitaka afanye naye kazi.

"Sanaa ni uelimishaji ndio maana tunasema ni kioo cha jamii kwa hiyo ambaye atanivunjia heshima kwa sababu nafanya maigizo huyo hakuwahi kuniheshimu tangu mwanzo,"amesema Abdul.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags