Linapokuja suala la historia Celine Dion yupo tayari kwa lolote

Linapokuja suala la historia Celine Dion yupo tayari kwa lolote

Mwanamuziki mkongwe wa Canada Celine Dion afunguka kuwa linapokuja suala la historia yake yupo tayari kwa lolote.

Mkali huyo wa ‘My Heart Will Go On’ akizungumza na ‘Smooth Radio’ baada ya kumaliza kutumbuiza kwenye michuano ya Olimpiki wiki iliyoisha amedai kuwa msanii unapokuwa na nyimbo nyingi na kuwa kimya muda mrefu hivyo lazima kukumbukwa na mashabiki.

“Kama wewe ni mshiriki au mwimbaji wa kundi lolote la kitambo na ukiwa umebahatika nyimbo zako kufuatiliwa zaidi unapokuja kuwa kimya kwa muda kidogo mashabiki wanakukumbuka muda wote, hivyo basi nahisi kukumbukwa sana na mashabiki wangu”

Aidha kwa kumalizaia ni ngumu kuzungumza jambo hili lakini anaamini kuwa linapokuja suala la historia yupo tayari kwa lolote lile.

Julai 26, 2024 Céline Dion alirudi tena jukwaani katika ufunguzi wa mashindano ya Olimpiki 2024 jijini Paris nchini Ufaransa, baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa stiff-person syndrome, uliopelekea kustopisha shughuli zake za kimuziki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags