Kumbe Lile Tumbo La Nyigu Sio Mimba Ni Kitambi

Kumbe Lile Tumbo La Nyigu Sio Mimba Ni Kitambi

Dansa maarufu Bongo, Angel Nyigu amezua gumzo mitandaoni baada ya kuonekana kuwa na tumbo kubwa kupitiliza.

Kutokana na kitambi hicho mara moja kuna taarifa zilisambaa kwamba huenda mwanamama huyo ni mjamzito na watu wengi ndiyo maana tumbo limemtoka hivyo au kama ni kuridhika na maisha basi ameridhika.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Mwanaspoti na kuulizwa kuhusiana na madai kwamba ni mjamzito, Angel alikuwa na haya ya kusema.

"Jamani sina ujauzito, hili tumbo ni kwamba nimenenepa tu, yaani nimeridhika na maisha ninayoishi lakini kama watu wananichuria haina shida kwa sababu kuzaa ni jambo jema sana."

Mashabiki wengi walionekana kuuponda muonekano wa Angel na kumkosoa kwa kujiachia na kunenepeana tu na kupoteza mvuto wake kama dansa.

Angel Nyigu ni dansa maarufu ambaye hucheza katika video za wasanii mbalimbali hasa wa Bongofleva, ameshawahi kutumika kucheza katika lebo ya WCB na kwa msanii Ali Kiba, Rayvanny na wengine wengi. akini wakati mwingine akiwa jukwaani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags