Usiyoyajua Kuhusu Manyanya Wa Dunia

Usiyoyajua Kuhusu Manyanya Wa Dunia

Mwigizaji wa tamthilia ya Dunia, Ally Mchonga ‘Manyanya’ amefichua kuwa mbali na uigizaji pia ni mwanamuziki na ameshawahi kutoa ngoma.

Akizungumza na Mwanachi Scoop, Manyanya amesema kabla hajatambua kipaji chake cha kuigiza alikuwa anaamini siku moja atakuwa mwanamuziki maarufu.

“Nilikuwa najua melodi za uimbaji pia nilikuwa naelewa sana kufanya rap kuna baadhi ya kazi ambazo niliachia YouTube. Nilitoa wimbo ulioitwa ‘Don’t Forget About’.

“Nafikiri hicho ndio kipaji chingine ambacho mashabiki hawakifahamu. Nafikiri siku za mbeleni nitaonesha uwezo wangu, mimi ni rapa mzuri sana na sio kama najisifia huo ndio ukweli,”amesema Manyanya

Alivyoanza kuigiza
“Historia yangu ilianzia mtaani sikujua kama ninajua kuigiza. Kulikuwa na rafiki yangu ambaye anapenda kuigiza ndio alinipa hamasa, nakumbuka siku moja kulikuwa na Audition Kwa Aziz Ally nikaenda naye kuangalia.

“Nikajikuta navutiwa kuona watu wakiigiza, mwongozaji wa audition hiyo alichagua ‘sini’ wote waliokwenda walishindwa kuifanya vizuri baada ya muda nikaomba kujaribu. Kila mtu alipiga makofi baada ya kumaliza kucheza ile sini. Kuanzia hapo nikajua nina kitu katika uigizaji,” amesema Manyanya

Aidha ameeleza baada ya kungundua kipaji chake aliamua kwenda shule kwa ajili ya kupata elimu kamili kuhusu uigizaji.

”Kuna darasa moja mbalo lipo Tandika linaitwa ‘Vision Talent’. Nikajifunza sanaa huko, mbinu za uigizaji. Lakini baada ya miaka miwili nikawa tayari kufanya kazi yoyote nikaanza kutafuta fursa.

“Kuna siku kukawa kunahitajika wasanii kutoka kampuni ya ‘Bichwa Production’ ambayo inaongozwa na Baba Asma. Nikaenda nilifanikiwa kupitishwa, tukaanza kuigiza tamthilia ya ‘Familia ya Mzee Kicheche’ na hii Dunia ni ya tatu,”amesema

Aidha amefunguka kuhusiana na baadhi ya mashabiki kumlinganisha tabia alizonazo katika Dunia Series.

“Kiukweli havina uhusiano sana na havina tofauti kubwa. Kuna baadhi ya tabia ninazo na kuna baadhi sina kabisa mfano tabia za upendo na mapenzi ninayo niko romantic sana, Pia niko serious,”amesema Manyanya

Licha ya kufanya vizuri kwenye Dunia Manyanya ambaye ni mwongozaji msaidizi kwenye tamthilia hiyo amesema kwa sasa bado hajapata mchongo wowote kutoka kwa watayarishaji wakubwa wa filamu nchini.

“Kwenye Dunia nina makubaliano ya muda mrefu. Kwa hiyo ukisema umtoe Manyanya ni kwamba unaenda kutengeneza mpasuko, lazima watu wakae mezani kufanya mahesabu ambayo yatasaidia pande zote mbili,”amesema

Mbali na hayo amefunguka kuhusu mahusiano yake huku akiweka wazi kwasasa yupo single.

“Lakini nina mtoto mmoja ni binti mwenye umri wa miaka 8. Nilimpata na mwanamke ambaye tulikuwa kwenye mahusiano kwa ufupi naweza kusema jimbo lipo wazi,”amesema Manyanya

Kuhusu jina la Manyanya
“Jina la manyanya nilipewa tangu nikiwa mdogo kama jina la utani. Nilivyokuwa nikaona nilichague kuwa jina langu la sanaa,”amesema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags