Kombe la Dunia lazua Ghasia Ubelgiji baada ya timu ya taifa kushindwa na Morocco

Kombe la Dunia lazua Ghasia Ubelgiji baada ya timu ya taifa kushindwa na Morocco

Polisi wa Ubelgiji wametumia nguvu kuyatawanya makundi ya watu katika mji mkuu Brussels katika ghasia zilizozuka kufuatia timu ya taifa ya nchi hiyo kugaragazwa na Morocco katika mechi ya kombe la dunia kwa mabao 2-0. Wafanyafujo walivunja vioo vya madirisha na kuyachoma moto magari huku wakirusha fashifashi.

Video moja iliyosambazwa mitandaoni imeonyesha watu hao wakilipindua gari jekundu kabla ya kulichoma moto. Rabsha rabsha ziliripotiwa pia katika miji mingine yenye watu wengi nchini Ubelgiji ya Liege na Antwerp. Nchini Morocco, umati wenye furaha ulijimwaga kwenye mitaa ya mji mkuu, Rabat kushangilia ushindi wa timu yao.

Katika mechi nyingine ya Kombe la Dunia, Ujerumani imetoka sare ya bao 1-1 na Uhispania na kubakisha hai matumaini ya kunusurika katika kundi E. Awali Costa Rica iliifunga Japan goli 1-0 kwenye mechi nyingine ya kundi hilo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags