Klabu maarufu kutoka nchini Saud Arabia, Al-Nassr anayocheza mwamba Cristiano Ronaldo imepigwa marufuku kusajili wachezaji wapya baada ya kushindwa kulipa stahiki za malipo ya nyongeza (add-ons) kutokana na usajili wa Ahmed Musa ambaye alijiunga na klabu hiyo kwa ada ya Pauni milioni 14 mwaka 2018.
Kwa mujibu wa Sport Tiger inaeleza kuwa FIFA iliwaonya Al-Nassr mwaka 2021 kwamba watakumbana na adhabu ya kufungiwa usajili ikiwa hawatailipa Leicester Pauni 390,000 kama nyongeza zinazohusiana na usajili wa Ahmed Musa baada ya mshambuliaji huyo kufanikiwa kushinda kombe la Ligi kabla ya kuachwa mwaka 2020.
Hivi sasa inaripotiwa kuwa FIFA imewafungia Al-Nassr kusajili wachezaji wapya na marufuku hiyo inaweza kudumu kwa takribani madirisha matatu ya usajili.
Huku mfuko wa Uwekezaji wa Umma (PIF) tayari umeweka wazi kuwa uko tayari kulipa ada hiyo ili kuondoa marufuku hiyo.
Leave a Reply