Kisa Klopp, Guardiola atoa machozi

Kisa Klopp, Guardiola atoa machozi

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola jana alimwaga machozi baada ya kuulizwa swali kuhusu kuondoka kwa meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp.

Klopp jana aliiongoza Liverpool kwenye mchezo wa mwisho na kuachana na ‘timu’ hiyo, akiwa anasema kuwa anataka kwenda kupumzika.

Guardiola aliiongoza City kutwaa ubingwa wa sita ndani ya misimu saba jana baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya West Ham ambapo timu yake ilifikisha pointi 91 mbili mbele ya Arsenal iliyomaliza nafasi ya pili.

"Nitammisi sana, Jurgen amekuwa mtu muhimu sana kwenye maisha yangu ya soka, amenifanya niwe kwenye levo nyingine kwenye maisha yangu.

"Nafikiri tunaheshimiana kila siku na ni mtu wangu wa karibu sana, naona bado anaweza kurudi, nataka kumshukuru sana kwa maneno yake," amesema Guardiola huku akifuta machozi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags