Kijana akamatwa baada ya kumrushia yai Mfalme Charles III

Kijana akamatwa baada ya kumrushia yai Mfalme Charles III

Mwanamume mmoja amekamatwa baada ya mayai kurushwa kwa Mfalme na Malkia Consort wakati wa ziara ya York, Uingereza. Kijana huyo mwenye miaka 23, alisikika akipiga kelele "nchi hii ilijengwa kwa damu ya watumwa," huku akizuiliwa.

Mfalme Charles aliendelea kupeana mikono na watu mashuhuri akiwemo Bwana Meya huku mayai yakiruka kuelekea kwake, akatulia kwa muda kidogo kuangalia maganda yaliyopasuka chini.

Mayai hayo yaliwakosa Mfalme na mkewe Malkia Consort. Tukio hilo lilitokea siku ya pili ya ziara rasmi ya kifalme huko Yorkshire.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags