Kesi 35 za Ukatili wa kijinsia zafikishwa Mahakamani Katavi

Kesi 35 za Ukatili wa kijinsia zafikishwa Mahakamani Katavi

Jumla ya kesi 35 za ukatili wa kinjinsia na unyanyasaji wa watoto Mkoani Katavi zilipata mafaniko mahakamani katika kipindi cha mwezi Januari hadi Novemba 2022 ukilinganisha na kesi 27 zilizofanikiwa kipindi kama hicho mwaka 2021.

Akizungumza na Wanahabari Ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi ACP-Ali Makame amesema mafaniko hayo ni ongezeko la kesi 8 sawa na asilimia 29.6.

ACP Makame amefafanua kuwa,kesi za kubaka zilikuwa 16, kulawiti 4, kulawiti na kubaka kesi 2, shambulio la kudhuru mwili 30, kujeruhi 5, kutishia kuua kwa maneno 1, unyanyasaji wa watoto 1, kuzini na mahalimu 1 na kutoa lugha ya matusi kesi 2.

Katika kesi hizo kwa mwaka 2021 na 2022,jeshi la Polisi mkoani Katavi lilifanikiwa kuwafikisha watuhumiwa mahakamani na baadhi yao kupatikana na hatia ambapo walihukumiwa vifungo mbalimbali.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post