Kwa wapenda vitafunwa vya haraka na vitamu, hotdog imekuwa miongoni mwa chaguo lao hasa mijini huku ikiwakosha wengi kutokana na ladha yake. Hotdog ni chakula rahisi kinachoweza kupikwa nyumbani bila vifaa vya gharama kubwa.
Asilimia kubwa ya watu wanaotoka out mara nyingi hukimbilia chakula hichi si kutokana na gharama yake kuwa ndogo bali ni kutokana na umaarufu wake pamoja na ladha. Hivyo basi ukiwa kama msakatonge unaweza kutumia kitafunwa hicho kama chanzo cha kupata mapato. Na hivi ndiyo namna ya kuandaa.
MAHITAJI
- Soseji 5-10 (Inategemea utatengeneza mikate mingapi)
- Ngano kilo moja (kwa ajili ya kutengenezea mikate (hotdog buns)
- Siagi, hamira, hiliki, chumvi, maziwa au nazi
- Spinachi zile ndogo zanauzwa super market
- Tomato na Chilli
JINSI YA KUTENGENEZA NA KUANDAA
Kwanza kabisa utaanza na kutengeneza mkate ambao ndio kitu muhimu cha kuwa nacho katika kitafunwa hicho.
Utachukua bakuli kubwa utaweka ngano, siagi, chumvi kiasi, hamira, hiliki, maziwa au nazi. Utakanda unga wako mpaka uwe sawa kabisa hakikisha unakuwa mlaini.
Baada ya kukanda utauacha kwa dakika tano ili uweze kuumuka kiasi. Baada ya hapo utaanza kuukata madonge marefu kama ambavyo picha zinaonesha.
Utafanya hivyo mpaka utakapomaliza ngano yako yote, kisha utaacha tena kwa dakika 10 mara baada ya hapo uchachukua mikate yako utakwenda kuioka kwa moto mdogo mdogo.
Wakati mikate yako ikiwa jikoni utachukua sufuria utaweka maji kiasi kisha utatia soseji zako kwa ajili ya kuzichemsha, kisha utaziweka jikoni kwa dakika 5-10.
Ukimaliza nenda katizame mikate yako kama tayari itoe na uweke pembeni ili ipoke. Chukua soseji weka pembeni, spinachi yako, tomato vyote viwekee tayari kwa ajili ya kutengeneza hotdog yako.
Baada ya kuweka kila kitu tayari sasa hatua ya mwisho utachukua mkate wako utauchana katikati (kama ambavyo picha zinaonesha) kisha utatanguliza spinachi yako, harafu soseji, kisha utamalizia na tomato, chilli juu. Utafanya hivyo mpaka pale utakapo maliza mikate yako yote.
NB: Kama sio mpenzi wa kula mboga za majani mbichi basi unaweza kuondoa spinachi kisha ukaweka vitunguu pamoja na nyanya.
Leave a Reply