Jinsi ya kuimarisha nywele zenye dawa

Jinsi ya kuimarisha nywele zenye dawa

Aloooh niaje watu wangu!! Its Friday bwanaa, kama kawaida, and this is fashion hatulali bwana mambo ni hot hot. Kama kawaida hapa ni bandika bandua bwana, weka vitu, leta vitu mtu wangu.

Wiki hii bwana tutazungumzia jinsi ya kuimarisha nywele zenye dawa, kama mnavyofahamu warembo wengi kwenye hili bwana humwambii kitu lakini je unazitunza vipi na kuziimarisha nywele zako?

Mambo yasiwe mengi twende sawa bwana. Wengi wetu huwa tunadhani kuweka dawa na kufanya steaming ndio kutakuza na kufanya nywele zetu kuwa na afya, hivyo utakuta mtu ana weka dawa kila baada ya mwezi na kufanyia steaming kila baada ya week mbili. Hii ndio husababisha nywele kunyonyoka na kutokua na afya.

Dawa si nzuri sana kwa nywele zako hivyo unashauriwa kuweka dawa mara mbili au tatu kwa mwaka.

Hii ina maana uweke dawa kila baada ya miezi sita hadi minne. Lakini swali linakuja je katika kipindi hiko chote ambacho nywele zina oteana na kukua utafanyaje hili zisikatike? 

 Hizi ndizo tips muhimu za nini ufanye:

 Deep Condition – fanyia deep condition mara kwa mara, hii itasaidia kulainisha nywele zako na kuipa nywele afya, wakati unafanyia deep condition ni vizuri ukaosha nywele na maji ya baridi na pia usikae kwenye moto, paka condition yako funga mfuko wa plastic na taulo juu kaa nalo kwa nusu saa osha.

Paka mafuta ya nywele kila siku – hii ni muhimu mno kwa nywele zako uli kuzipa nywele unyevu na kulainisha ili kuzuia ukatikaji wa nywele ni muhimu uwe unapaka mafuta mara kwa mara, na mafuta mazuri kwa ajili ya nywele ni mafuta ya kumiminika na si mafuta ya mgando. Eg olive oil ya maji au mafuta ya nazi ya maji.

 Kata ncha- Kukata ncha kunasaidia ukuaji wa nywele pia husaidia kujaza nywele.

Suka misuko ambayo haikati nywele – ipo mingi sana unaweza ku google “protective hair styles” ukaipata lakini pia nywele za kurudi nyuma “twende kilioni” husaidia mno ndio maana utakuta wanafunzi wengi wana nywele ndefu zilizo na afya.

Punguza kukaa/kutumia vitu vya moto – kutumia pasi au dryer kukaushia au kunyooshea nywele mara kwa mara kuna athiri nywele, nywele hupoteza ubora wake kutokana na moto. Hii huathiri hata zile nywele zinazoota. Kama unaosha nywele mara kwa mara ni vyema ukaziacha zikauke zenyewe na upepo.

Eiwaaaah. I hope tumeelekezana vizuri kabisa mazingatio, ni juu yako mrembo hakikisha unafuata maelekezo ili uweze kujiimarisha na kuwa bora zaidi happy wikiend guys!!!

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post