Je wajua ni kosa KUUZA MAJI

Je wajua ni kosa KUUZA MAJI

Kama ulikuwa haujui, basi wacha leo nikujuze.

Je wajua kuuza maji ni kosa? Basi bwana kama una kisima chako cha maji na unawauzia majirani bila utaratibu, ipo siku unaweza kuishia pabaya!

Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi WRBWB (Bodi ya Maji, Bonde la Wami Ruvu), Mhandisi Elibariki Mmasi akizungumza katika kipindi cha runinga moja nchini.

Mhandisi alinukuliwa, "Kuna mtu ana kisima anafanya shughuli za kibiashara kama 'car wash', hotel, kituo cha mafuta, yule mwenye kisima akaamua kuwauzia majirani zake maji anachofanya ni kosa. Hatumzuii kutoa huduma Ila anatakiwa kufuata taratibu. Unaweza kuwa na kisima cha maji lakini majirani zako wana wakati mgumu unatakiwa wale majirani uwapatie maji. Kama unahitaji kufanya biashara ya maji unatakiwa uombe kibali kwetu ili usajiliwe." 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post