Na Habiba Mohamed
Niaje niajeeeeeeeee watu wangu wa nguvu, kama ilivyokawaida nyota njema huonekana asubuhi, basi bwana msanii na mfanyabiashara maarufu Roby Rihanna Fenty ambapo jina lake la kutafutia ugali wengi wenu mnamfahamu kama Rihanna,
Rihanna amezaliwa visiwa vya Barbados na kutokana na mafanikio yake ya biashara ya mavazi na mziki amepewa thamani kubwa katika taifa hilo kwa kuwekwa siku maalumu ya mapumziko ambapo Waziri mkuu Mia Mottey alimtangaza rasmi kuwa mwanamuziki huyo ni shujaa wa taifa hilo na siku hiyo ikiwa ni sikukuu ya kitaifa.
Licha ya kuwekwa siku hiyo vile vile pia katika mji huo kuna mtaa umepewa jina la ‘Rihanna drive’ kama heshima ya kulitangaza taifa hilo duniani kupitia taranta yake ya uimbaji na mitindo.
Hii imekuwa tofauti na msemo wa ‘nabii hakubaliki nyumbani kwao’ maana Rihanna amejizolea umaarufu katika visiwa vya Barbados na ulimwenguni kote.
Aidha huko marekani Makavazi ya Metropolitan museum of Arts imechonga sanamu ya picha ya Rihanna kuonyesha ukubwa wake katika tasnia ya mzikii na mitindo, bwana weeeh huyo ndo yule dada wa ‘shine bright like Diamond’
Duuuuuuuh! Haya sasa turudi kibongo bongo unafikiri msanii yupi anastahiri kupewa heshima kitaifa kupitia tasnia yake katika kuitangaza nchi ya Tanzania ulimwenguni, Shusha comment yako hapo chini.
Leave a Reply