Ebanaee!! Mambo ni mengi muda mchache wanetu basi bwana tasnia ya muziki huu wa kizazi kipya (Bongo fleva) kumekuwa na mtindo ili msanii atoke au afanikiwe basi afanye jambo kubwa litakalo washangaza watu (kiki) tofauti na zamani ilikuwa nyimbo ikiwa nzuri basi ndio msanii atatoboa na kuwa maarufu yani kazi yako kali ndio ilikuwa inakutambulisha.
Masanii maarufu wa hip hop, Izzo Bizness kupitia mahojiano yake na moja ya chombo cha habari alifunguka na kueleza kuwa siku hizi kila mtu anamtindo wake katika sana ya muziki tofauti na zamani.
“Wakati wetu sisi ilikuwa ili utoke kimuziki lazima uwe na ngoma kali na uumize kichwa kutengeneza muziki mzuri na kulikuwa hakuna haja tena ya kupush mziki wako, ngoma ilikuwa inaenda yenyewe kwa sababu ni nzuri” Aliendelea kusema
“Nitofauti na sasa hivi kwanza ukiachana na mtu kutoa nyimbo kali hatakama ni mabadiliko ya generation lakini imewekeza zaidi kwenye matukio au jambo la kutengeneza attention ndio mtu afanye project yake” alisema Izzo B.
Mwisho aliwataka wanamuziki wanao chipukia kuwa na heshima katika kutengeneza mziki ilikudumisha uaminifu kwa fans nasio kutafuta kiki.
Leave a Reply