Hizi hapa flat shoes zitakazo kufanya uwe namuonekano mzuri zaidi

Hizi hapa flat shoes zitakazo kufanya uwe namuonekano mzuri zaidi

Hellow its Friday mtu wangu karibu sana kwenye kipengele cha fashion kama kawaida yetu huu ndio ukurasa pekee unaoweza kukusaidia wewe mpenda mitindo kuhakikisha muonekano wako unazidi kuwa bora.

Wiki hii kwenye kipengele hiki tutakwenda kudadavua aina kadhaa za Flat shoes zitakazokufanya uwe na muonekano mzuri zaidi karibu

Nikukumbushe kuwa  kuna aina nyingi sana za viatu ambavyo ukivaa vitakufanya uwe na muonekano mzuri kama unavyojua kuwa kiatu ndio kitu ambacho kinafunga muonekano wako, ukikosea kwenye kiatu utafanya muonekano wako wote kuharibika na ukipatia basi kinanyanyua muonekano wako kwa kiasi kikubwa.

Haswaa nikwambie tu kuwa wapo watu ambao hawawezi kuvaa heels kutokana na sababu mbalimbali, kama ulikua unafikiri heels ndio kiatu pekee kwa kuweka muonekano mzuri basi soma hii hap tukianza na aina ya kwanza ya flat shoes.

  • Mules shoes

Bwana kiatu hiki kilianza kuvaliwa kipindi cha rome but now kipo kwenye trends na kimeteka sana dunia. Mules shoes ni aina ya kiatu ambacho ukivaa unajifeel comfortable na classy kitu ambacho kinakufanya uwe na muonekane mzuri ukivaa iko kiatu ni kwa sababu kinachukua attention ya muonekano wako wote na ukiwa umevaa palazzo itakufanya uoekane vizuri kabisa.

  • Brougues shoes

Hiki ni aina ya kiatu ambacho ukivaa kitakufanya uonekane vizuri kwa sababu kinacover sehemu kubwa ya mguu. Brougues ni kiatu ambacho unaweza kuvaa na aina nyingi ya mitoko unaweza ukavaa na short loose dress na ukaonekana elegants na mtu ambae unaenda na fashion. Pia aina hii ya kiatu unaweza ukavaa na jeans kwa sababu mastar wengi wa nje upendelea kuvaa ivo na bado ukazidi kuonekana more elegant & stylish.

  • Ballet flats

Kuna aina nyingi sana za flats shoes ila ballet flats ni aina ya kiatu ambacho kinakufanya uonekane elegant kwa extra mile, ballet ni classy, comfy, elegant na perfect kwa kuvaa kila siku.


Loafers

Unaambiwa loafers shoes ni simple to get on and off. Loafers vipo katika materials tofauti tofauti kama leather, rubber, suede, wool. Kwasasa watu wengi hupenda kuvaa loafers kama casual wear, lounge wear na hata business wear na vitakufanya kuonekana elegant kwa muda wote na kuwa comfortable kwa shughuli za siku nzima za kikazi pia

Ebwana eeeh kwa leo mimi nimekomea hapo bwana lakini unaweza kujiongeza pia kama utaona aina nyingine basi utaruka nayo bwanaa furahia kipengele hiki kwa kuimarisha muonekano wako.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags