Hawa ndio mastaa wanaokimbiza Spotify

Hawa ndio mastaa wanaokimbiza Spotify

Na Asma Hamis 

Mwaka 2024 umeleta mafanikio makubwa kwa wanamuziki wengi wa rap duniani, huku baadhi yao wakivunja rekodi za kusikilizwa zaidi kwenye mtandao wa Spotify.

Wasanii wakubwa wa rap wameendelea kuonyesha umahiri wao, na baadhi yao wametawala majukwaa kwa muda mrefu, wakati wengine wameibuka na kushangaza wengi. Kwa mujibu wa tovuti ya spotify na hawa ndio wasanii waliopata wasikilizaji wengi kwa mwaka 2024.

Drake
Msanii anayeongoza katika listi ni mwanamuziki kutoka Canada, Drake ambaye mpaka kufikia sasa anawasikilizaji zaidi ya bilioni 13.7, rekodi hiyo inakuja kufuatia na ngoma zake zilizochanganyika rap, R&B, albumu pamoja na kuandika mistari inayolengana na maisha halisi ya watu.

Travis Scott
Namba mbili inaenda kwa mzazi mwenzie na Kylie Jenner, Travis akiwa na zaidi ya wasikilizaji bilioni 10, msanii huyu anajulikana kwa sauti nzuri na mchanganyiko wa nyimbo zake za rap na hip hop, huku akiwavutia zaidi mashabiki kwenye majukwaa mbalimbali ya fashion.

Kanye West
Ukiachana na mapenzi yake kwenye fashion na mitindo West pia ni miongoni mwa wasanii kutoka Marekani wanaokimbiza ambapo kwasasa kupitia mtandao wa Spotify ana zaidi ya wasikilizaji bilioni 9.3.

Ingawa Kanye mara nyingi hupata mijadala mingi kuhusu matamshi yake, ila uwezo wake wa ubunifu haujadiliki, na bado ana mashabiki wengi wanaosikiliza nyimbo zake kupitia Spotify.

Future
Uwezo wake wa kutunga mashairi yanayogusa hisia za wasikilizaji zinaendelea kumfanya Rapa Future kubaki kuwa msanii namba nne anayesikilizwa zaidi kupitia mtandao wa Spotify ambapo mpaka kufikia sasa anaziaidi ya wasikilizaji bilioni 7.9 kupitia mtandao huo.

Kendrick Lamar
Mbali na kufanya kazi nyingi mwaka huu ambazo zilihusisha moja kwa moja bifu lake na Drake lakini mwamba huyo ameendea kujiweka katika nafasi nzuri katika mtandao wa Spotify kwa kuwa na zaidi ya wasikilizaji bilioni 7.8.

Mbali na hao nguli watano ambao wanautikisa mtandao wa Spotify kwenye Rap lakini wapo wengine ambao bado wanajikokota kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mtandao huo akiwemo…

Eminem (bilioni 7.8), 21 Savage (bilioni 6.4), Playboi Carti (bilioni 5.0), Nicki Minaj (bilion 4.3), Doja Cat (bilion 4.1), J. Cole (bilion 3.8), Lil Baby (bilioni 3.7) na wengineo.
Spotify imeendelea kuwa jukwaa muhimu linalowaunganisha mashabiki kote duniani, na mwaka 2024 umeonekana kuwa wa mafanikio kwa rappers hao, kutokana na kuleta radha mbalimbali katika tasnia ya burudani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags