Hatima ya Diamond kwenye Tuzo za Grammy kujulikana kesho

Hatima ya Diamond kwenye Tuzo za Grammy kujulikana kesho

Na Asma Hamis

Zimebaki zimebaki saa chache dunia ishuhudie majina ya mastaa watakaowania tuzo kubwa za muziki nchini Marekani 'Grammy', nyota wa ‘Komasava’ Diamond naye ni miongoni mwa wasanii wanaosubiri majina yao kutajwa.

October 11, 2024 Diamond aliwasilisha majina yake kupitia wimbo wa 'Komasava' katika vipengele viwili, kwanza Video Bora (Komasava) na Mtumbuizaji Bora kutoka Afrika.



Hata hivyo baada ya wasanii kuwasilisha majina yao waandaaji wa tuzo hizo walitangaza kuwa Novemba 8, 2024 wataachia majina ya watakaowania tuzo hizo msimu wa 2024/2025, huku mastaa kutoka mataifa mbalimbali wakiwasilisha kazi na majina yao ili kuondoka na tuzo hizo, ambazo zinatarajia kutolewa Februari 2, 2025.

Wimbo ambao Simba ameuingiza kwenye kinyang’anyiro hicho huenda ukatajwa kuwania tuzo za Grammy kutokana na kuwa na rekodi nyingi za mafanikio, moja wapo ikiwa ni wimbo huo kuingia katika chati za Billboard.

Hii sio mara ya kwanza kwa msanii Diamond kuingiza nyimbo zake katika tuzo hizo, utakumbuka kuwa mwaka 2020 aliingiza wimbo wake wa ‘Jeje’ katika Kinyang’anyiro hicho na kuishia hatua ya kwanza iitwayo ‘Consideration’.

Hata hivyo, kwa mwaka huo Diamond hakuwa peke yake alikuwa na wasanii wenzake kama Zuchu na Rayvanny, Zuchu akiingia kama Mwanamuziki Chipukizi, Simba akiingia kwenye Video Bora ya Mwaka kupitia video ya Baba Lao na Jeje na Rayvanny akiingia kwenye Album Bora ya mwaka Duniani kupitia EP yake ya Flowers.

Rayvanny aliteuliwa kwenye Tuzo za Grammy katika kipengele cha Albamu Bora ya Pop ya Kilatini kutokana na ushirikiano wake na mwimbaji wa Colombia Maluma kwenye wimbo wao “Mama Tetema” ambao awali ulitengenezwa na Rayvanny akimshirikisha Diamond Platnumz huku mtayarishaji akiwa S2Kizzy ‘Zombie’.

Ikumbukwe kati ya wasanii kutoka Afrika waliowahi kushinda Grammy ni Tyla kutoka Afrika Kusini na hata Burna Boy kupitia albamu yake ya tano 'Twice as Tall' (2020) aliyoshinda kama Albamu Bora ya Muziki Duniani 2021 na kuandika rekodi kuwa msanii wa kwanza wa kiume Nigeria kushinda Grammy kupitia kazi yake mwenyewe.

Remix ya wimbo wa ‘Komasava’ mpaka kufikia sasa ina zaidi ya watazamaji milioni 27 katika mtandao wa YouTube huku original yake ikiwa na watazamaji milioni 6.5.






Comments 1


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post