Baada ya kuwepo na maneno katika mitandao ya kijamii kuhusiana na mwanamuziki Harmonize kuhusishwa kutoka kimapenzi na mfanyabiashara Malaika hatimaye msanii huyo ametoa ya moyoni huku akiwataka watu wamchagulie mtu wanayeona anamfaa.
“Hatuna misingi ya Ubaya Ubwela siridhishwi na baadhi ya kauli mbaya tena zinazomlenga mtoto wa kike, kisa tu amechagua kuwa yeye au aliteleza hapo nyuma watu tunatupia mengi hata mimi nishakosea watu na wakanisamehe, tena mnaambatanisha na umbo lake maridhawa alilolichagua mnamsema nao that not nice.
“Nilitegemea nyinyi muwe mstari wa mbele kuiomba Serikali impatie ulinzi malighafi anazotembea nazo mwilini sio wa kuzunguka zunguka na Mwijaku siku akihama nchi mtaanza kusema oooh wakwetu wakwetu nishashuhudia watu kadhaa wakiathirika kisa kusemwa, kila mtu yupo huru kuwa anavyotaka nothing wrong with that, sawa nishawaambia ni mshikaji wangu, haya nichagulieni basi huyo mnayeona anafaa,” ameandika Konde Boy kwenye ukurasa wake wa Instagram
Utakumbuka kuwa Konde na Malaika wanahusishwa kutoka kimapenzi kwa siku za hivi karibuni baada ya kuonekana pamoja ndani ya wiki kadhaa huku mwanadada huyo akionekana kwenye video ya wimbo wa Marioo aliyomshirikisha Harmonize uitwao ‘Wangu' uliotazamwa zaidi ya mara laki mbili kwenye mtandao wa YouTube.
Leave a Reply