Harmonize na Libianca kwenye ngoma moja

Harmonize na Libianca kwenye ngoma moja

Mkali wa Bongo Fleva, Rajab Kahali, ‘Harmonize’ yupo mbioni kuachia video ya ‘Side Niggah’ remix aliyomshirikisha mwanamuziki kutoka Cameroon Libianca Kenzonkinboum.

Mkali huyo wa ngoma ya 'Single Again' amethibitisha ujio wa ‘kolabo’ hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiwataka mashabiki kukaa mkao wa kula.

Utakumbuka kuwa Libianca aliwahi kutamba na ngoma yake ‘People’ aliyoiachia mwaka 2022, wimbo ambao ulifanya vizuri na kushika nafasi ya pili kwenye chati ya Billboard Afrobeat nchini Marekani pamoja na chati ya Afrobeats nchini Uingereza.

Wimbo wa ‘Side Niggah’ unaotarajia kutolewa remix, umetoka kwenye album ya Harmonize ya 2023 ya ‘Visit Bongo’ albumu hiyo iliyojaa vibao kama vile ‘Single Again’, ‘Dear X’,‘Boss,’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags