Harmonize ampa nguvu Dulla Makabila

Harmonize ampa nguvu Dulla Makabila

Mwanamuziki wa singeli #DullaMakabila ametoa shukurani kwa msanii wa bongo fleva #Harmonize baada ya #Konde kueleza kuwa wimbo wa singeli kuwa hit Tanzania ni wa #Dulla.

#Harmonize kupitia mahojiano yake na moja ya chombo cha habari nchini ameeleza kuwa wimbo ambao uliwahi kuwa hit ni ‘Pita huku’ wa #DullaMakabila, jambo ambalo lilimpa nguvu #Makabila na kutoa shukurani zake kwa msanii huyo. Dulla ameandika,

“Kwanza pongezi kwa tuzo zako ambazo zimeiletea heshima nchi yetu. Pili nashukuru kwa kutambua kazi yangu japo wengi wanafahamu umuhimu wa wimbo wa ‘Pita huku’. Siyo kila mtu anaweza kuheshimu hilo, asante sana kaka. Hii imenipa nguvu zaidi ya kuendelea kupeperusha bendera ya waimbaji”.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags