Haji Manara amchumbia Zaylissa

Haji Manara amchumbia Zaylissa

Aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara, amvisha pete ya uchumba mpenzi wake Zaylissa siku ya jana Januari 18.

Sherehe hiyo ya kuvishana pete ilienda sambamba na kusherehekea kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Haji, ambapo ilihudhuliwa na mastaa mbalimbali akiwemo Aunty Ezekiel, Arene Uwoya, Diamond, Lamata, Nandy, Ommy Dimpoz na wengineo.

Katika sherehe hiyo Haji ametoa ya moyoni kwa kusema kuwa anaomba sana dua za mashabiki wao kwani anatamani ndoa anayotarajia kufunga na Zai iwe ya mwisho kwake.

Zay na Haji walianza kuhusishwa kwenye uhusiano wa kimapenzi mapema mwezi November mwaka jana, ingawa mwanzo waligoma na kudai kuwa wapo kwenye urafiki wa kawaida.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags