FANYA MAZOEZI HAYA UKIWA NYUMBANI

FANYA MAZOEZI HAYA UKIWA NYUMBANI

Sio kila mtu anapenda kufanya mazoezi Gym. Wengine kama mimi tunapenda kufanya mazoezi nyumbani kwa sababu moja au nyingine.

Na kama wewe unaangukia kundi hii, fuata hatua hizi 5 za kufanya mazoezi nyumbani:

  1. Andaa nafasi maalum

Unahitaji nafasi maalum kufanya mazoezi, ili uweze kuyafanya bila shida, kwa hiyo, hakikisha una nafasi isiyopungua futi 5 kwa futi 5.

Tunasema nafasi ni muhimu kwa sababu mazoezi mazuri yanatakiwa yafanye sehemu yenye uwazi kidogo ili kuzuia mtu asiweze kuumia.

  1. Tumia chochote kile!

Ndio tumia kitu chochote iwe ukuta, ngazi, viti, hata kikapu cha nguo chafu! Unaweza ukatumia vifaa hivi kwa mazoezi. Kwa mfano:  Panda na kushuka kwenye ngazi mara nyingi, beba fagio kwa usawa ukiwa una ruka kichurachura, shika ukuta halafu ruka kichurachura.

  1. Vifaa muhimu

Ukiwa unahitaji kufanya mazoezi nyumbani hakikisha unakuwa na vifaa vingine muhimu kwa ajili ya kazi hiyo kama kamba, vifaa vya chuma, mpira na vinginevyo.

Vifaa hizi muhimu vitakurahishia katika ufanyaji wa mazoezi yako kaka au dada ambaye hupendi kabisa kwenda Gym.

  1. Jifunze mazoezi ya kawaida

Kwa kuwa utakuwa unafanya mazoezi nyumbani, mazoezi ya kawaida ndio yatakusaidia sana, zikiwemo, Sit up, Push up, Kuruka kichurachura, Step up, Crunches

  1. Mashine za mazoezi

Kama una uwezo unatakiwa kuwa na treadmill (mashine ya kukimbia), baiskeli ya mazoezi na mengineyo yanaweza kukupa motisha zaidi kufanya mazoezi. Ukiwa nayo, kuna uwezekano mkubwa wa kwamba utaitumia.

Kwenya suala la mazoezi, kuanza ndio ngumu zaidi vitu vyote vingine. Kwa hiyo, usifikirie sana. Amka kesho asubuhi alafu fanya mazoezi ya kawaida kwa dakika 30. Endelea hivyo kidogo kidogo mpaka itakapozoea.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags