Fahamu kuhusu biashara ya kuosha magari (carwash)

Fahamu kuhusu biashara ya kuosha magari (carwash)

Hellow! Niaje niaje wanangu wa Mwananchi Scoop. I hope mko byee kabisa, haya wale wanangu wa kuchakarika wajasiliamali yaani tushasema sisi na biashara mpaka mtuue. Leo bwana kwenye segment yetu pendwa tunakusogezea mada ambayo baadhi ya watu hawakuitegemea kabisa.

Biashara ya kuosha magari siku zote huwa na faida kubwa sana, uzuri wa hii uwe na mtaji mdogo ama mkubwa itakua tu na wewe mwenyewe utashangaa.

Kuna huu msemo unasema kuwa kuna watu hutumia wakati kuokoa pesa na kuna watu ambao hutumia pesa kuokoa wakati. Unapoanza biashara ya kuosha magari, kimsingi unalenga watu ambao wanahitaji kutumia pesa kuokoa muda.
 

Tuseme tu ukweli, sio kila mtu ana wakati wa kuamka asubuhi na mapema na kuosha gari lake kabla ya kuanza majukumu ya kila siku. Hata ikiwa watafanya hivyo ni kazi kubwa kusafisha eneo la ndani na kuosha matairi yawe safi na gari kwa ujumla.

Katika uoshaji wa magari hutakiwi kabisa kukurupuka eti kisa umemuona fulani anaosha na wewe ufanye hivyo hivyo, cha kufanya ni kuanza kwa kujifunza kutoka kwa wataalamu. Tembelea huduma yoyote ya kitaalam ya kuosha magari unayojua na ujifunze chochote unachoweza kutoka kwao ili kupata ufanisi zaidi unaweza kujitolea kufanya kazi bure wakati unajifunza.

Ukishamaliza hapo, haya ndo mambo ya kuzingatia kama unahitaji kufungua sehemu ya kuosha magari (car wash):

  • Pata eneo zuri la kibiashara

Eneo ni muhimu sana kwa biashara ya kuosha gari. Eneo zuri ni nini?
Kwanza eneo lako linapaswa kuwa lenye shughuli nyingi na watu wanaopata mapato ya kutosha ambao wanaweza kumudu kulipia huduma yako. Hapa sasa ndo tunakuja na kauli yetu ile ya unawalenga watu wanaotumia pesa kuokoa muda.

Kwa hivyo, ukipata nafasi karibu na duka la magari ama fundi makenika, unaweza kuwa katika eneo zuri sana la kibiashara. Vivyo hivyo kwa maeneo yenye vumbi sana sio lazima kwenye maduka ya vifaa vya magari tu.


  • Hakikisha kuna maji ya kutosha

Kuosha gari inahitaji maji mengi mno ilikufanikiwa zaidi utahitaji chanzo cha kutosha cha maji, kwa hivyo zingatia eneo utakalochagua lisiwe na tabu ya maji kabisa maana biashara yako itadoda na utaiona chungu na ngumu.

Nimeona baadhi ya watu wanaofungua biashara ya kuosha magari karibu na kijito. Wengine hununua tanki kubwa la kuhifadhi maji na kujaza kila siku.

Jambo moja ninaweza kukuambia ni kwamba hupaswi kuwarudisha wateja wako kwa sababu ya kukosa maji, watakuona kama mtu usiye serious na kazi ama biashara yako.



  • Kununua vifaa vyenye ubora zaidi

Biashara ya kuosha gari ni kwamba unaweza kuianzisha kwa kiwango chochote cha mtaji, unaweza kuwekeza kiasi kikubwa cha pesa, ikiwa unaweza kuimudu kuanza uoshaji wa kisasa wa magari. Unaweza pia kupata ndoo mbili, kitambaa kimoja na sabuni na kuosha magari ya watu. Njia yoyote unayochagua, utapata pesa ikiwa utatoa huduma nzuri kadiri iwezekanavyo.

Pata vifaa unavyoweza kumudu katika biashara yako. Itaonesha wateja wako unajua na unathamini unachofanya kweli.

Baadhi ya vifaa unavyotakiwa kuwa navyo katika biashara hii ya uoshaji wa magari:

  • Pressure car washer
  • Towels
  • Brushes
  • Chemicals
  • Compressors
  • Conveyor
  • Mobile wash systems, etc


Ikiwa unaweza kununua vifaa hivi tangu unapoanza, sawa. Lakini ikiwa unaanza kidogo, ninashauri uwekeze pesa unayopata kupata vifaa bora kwa biashara yako.

Sasa ili uweze kutoboa kwa haraka ni kuongeza huduma. Unaweza kuongeza huduma kwa biashara yako ya kuosha gari ili kuongeza mapato. Unaweza kuongeza baa ndogo ili watu wapate kiburudisho wakati wanangojea gari lao. Unaweza pia kuongeza kituo cha kutazama michezo, duka la kubashiri (betting shop), n.k.

Haya haya, hii kazi sijamtaja mkaka au mwanaume hapo juu kama kawaida yetu siku hakuna kazi ya wanaume au vijana kazi ni kazi ilimradi mkono uwende kinywani. Fanya kazi nzuri, chukua tahadhari zaidi kulinda magari ya watu na kile kilichomo wizi mmoja, kashfa au utovu wa nidhamu utapelekea wateja wako kukukimbia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags