Drake Na Lamar Waingiza Mkwanja Mrefu 2024

Drake Na Lamar Waingiza Mkwanja Mrefu 2024

Wanamuziki wa Hip Hop ambao walitawala vichwa vya habari duniani kote Drake na Kendrick Lamar wametajwa kuwa ndio wasanii wa Rap walioingiza mkwanja mrefu zaidi mwaka 2024.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Laminate imeonesha kwamba bifu la wawili hao lililojikita kwenye kutoleana ngoma za madongo (Disstrack) limepelekea kukusanya jumla ya dola milioni 15.3 ndani ya miezi minne kwa wote wawili.

Kufuatia na ripoti hiyo imeonesha kuwa wimbo wa “Not Like Us” na “Like That,” kutoka kwa Lamar uliongoza kwa mapato ambapo ulikusanya dola milioni 7.6 na dola milioni 4.6 huku kwa upande wa Drake kupitia wimbo wa ‘Family Matters’ akiondoka na takibani dola milioni 2.

Bifu la wawili hao lilianza baada ya Lamar kutoa ngoma iitwayo ‘Like That’ akijitambulisha kuwa yeye ni bora kuliko Drake huku akidai kuwa amewazika mastaa wote wanaomuunga mkono Drake kupitia albumu yake ya ‘For All The Dog’.

Mbali na hilo lakini pia wapo baadhi ya mastaa walilifurahia bifu hilo akiwemo Snoop Dogg ambaye alidai kuwa bifu hilo limepelekea kurudisha tasnia ya muziki wa hip-hop katika mstari wake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags