Drake akubali kushindwa bifu lake na Lamar

Drake akubali kushindwa bifu lake na Lamar

Ikiwa umepita mwezi, bila mashabiki kusikia chochote kuhusiana na bifu la wasanii Drake na Kendrick Lamar, sasa inaonekana kama Drake amekubali kushindwa, baada ya kufuta maudhui yote aliyokuwa akimrushia madongo Lamar.

Drake amefuta jumbe zote ambazo zilimlenga Lamar hadi ngoma yake ya "The Heart Part 6," ambayo aliitoa kwa ajili ya kujibu ngoma ya Lamar ya ‘Not Like Us’ iliyovunja rekodi ya ‘The Boys’ kwenye mtandao wa Spotify.

Hata hivyo mwanamuziki huyo amechapisha picha mpya akiwa nje ya mjengo wake uliopo Toronto . Hata hivyo mashabiki kupitia upande wa kutuma jumbe, wameendelea kumcha Drake kwa kudai kuwa amefanya hayo kwa ajili ya kuzima tangazo la onesho lijalo la Lamar la Ken & Friends litakalofanyika Los Angeles, Juni 10. 

Bifu la wawili hao lilianza baada ya Lamar kutoa ngoma iitwayo ‘Like That’ akijitambulisha kuwa yeye ni bora kuliko Drake huku akidai kuwa amewazika mastaa wote wanaomsapoti Drake kupitia albumu yake ya ‘For All The Dog’.

Ikumbukwe kuwa rapa Snoop Dogg alionesha kufurahishwa na bifu la wawili hao huku akidai kuwa limepelekea kurudisha tasnia ya muziki wa hip-hop katika mstari wake, kwa kudai kuwa nyimbo walizokuwa wakizitoa kwa ajili ya kurushiana madongo zimeimarishwa kwenye uandishi.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post